Nov 27, 2021 08:03 UTC
  • Muhammad Islami: Waliojitoa JCPOA hawana haki ya kuzungumzia miradi ya nyuklia ya Iran

Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran amesema kuwa, waliojitoa katika makubaliano ya kimataifa ya nyuklia ya JCPOA hawana haki ya kuzungumzia na kueleza mitazamo yao kuhusiana na miradi ya nyuklia ya Tehran.

Muhammad Islami amesema hayo pambizoni mwa kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kuuawa shahidi Mohsen Fakhrizadeh mwanasayansi bingwa na mwenye kipawa cha juu katika masuala ya nyuklia na ulinzi wa Iran na kueleza kwamba, miradi ya nyuklia ya taifa hili ina mfungamano na suala la makubaliano ya nyuklia na wale ambao walikiuka ahadi na kujitoa katika makubaliano hayo ya kimataifa kwa sasa hawana haki ya kuzungumzia miradi ya nyuklia ya Tehran inayofanyika kwa malengo ya amani.

Mohsen Fakhrizadeh, ambaye alikuwa mkuu wa shirika la utafiti na teknolojia la Wizara ya Ulinzi ya Iran aliuawa shahidi Novemba 27, 2020 katika shambulio la kigaidi lililofanywa kwenye viunga vya mji wa Tehran.

Shahidi Mohsen Fakhrizadeh, aliuawa shahidi Novemba 27, 2020 katika shambulio la kigaidi katika viunga vya Tehran

 

Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran amesema kuwa, upande wa pili wa mazungumzo ya nyuklia na Iran haukutekeleza ahadi zake hususan katika kipindi cha uongozi wa Rais Donald Trump na hivyo kuheshimu makubaliano hayo hakuwezi kuwa ni suala la upande mmoja.

Kadhalika Muhammad Islami amesema kwamba, mazungumzo yajayo ya nyuklia ya Vienna Austria nayo ni kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na suala la upande wa pili kutekeleza ahadi zake kwa mujibu wa makubaliano hayo.

Duru mpya ya mazungumzo ya nyuklia  baina ya Iran na kundi la 4+1 kwa ajili ya kuondolewa vikwazo Tehran imepangwa kufanyiika tarehe 29 ya mwezi huu wa Novemba.

Tags