Nov 27, 2021 14:41 UTC
  • Tehran: Utawala wa Kizayuni ufikirie kwanza ukubwa wake kabla ya kufikiria kushambulia vituo vya nyuklia vya Iran

Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni unapaswa kufikiria ukubwa na udhaifu wake kwanza kabla ya kujipa uthubutu wa kutoa majigambo kuwa itashambulia taassi za nyuklia za Iran.

Mohammad Eslami amesema hayo katika mahojiano na televisheni ya al Masirah na kuongeza kuwa, katika mkakati wake wa kitaifa, kamwe Iran haijawahi kufuatilia silaha za nyuklia na haitofanya hivyo. Harakati za Tehran zinafanyika chini ya misingi ya sheria za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA.

Ameongeza kuwa, katika ukaguzi wote uliofanywa na IAEA kwenye taasisi za nyuklia za Iran, hakujaonekana sehemu yoyote ambapo Tehran imekwenda kinyume hata chembe na sheria za kimataifa, lakini ubeberu wa kimataifa unaona kuwa kama utawaua kigaidi wanasayansi wa nyuklia wa Iran basi utatoa pigo kubwa kwa Mapinduzi ya Kiislamu, wakati uhakika wa mambo ni kinyume kabisa na yanavyojidaganya madola hayo ya kiistikbari.

Bendera ya utawala wa Kizayuni wa Israel

 

Mkuu wa Taasisi ya Nyuklia ya Iran amesisitiza pia kuwa, ugaidi huo wa madola ya kibeberu si tu haukwamishi mradi wa nyuklia wa Iran, lakini unazidi kuwatia hamasa vijana wa Iran na kuwafanya waongeze jitihada za kuendelea na shughuli zao za amani za nyuklia.

Vile vile amesema, mazungumzo yanayokuja ya huko Vienna, Austria ni kwa ajili ya kuzirudisha pande zilizojitoa kwenye mapatano ya nyuklia ya JCPOA yaliyofikiwa huko nyuma, si mazungumzo kuhusu mradi wa nyuklia.

Tags