Nov 28, 2021 11:56 UTC
  • Raisi: Uhusiano unaoimarika kati ya Iran na Tajikistan utaendelezwa kwa nguvu

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa uhusiano mwema kati ya Iran na Tajikistan utaendelezwa kwa nguvu zote katika nyanja za kibiashara, kiutamaduni na kiuchumi.

Rais Sayyid Ebrahim Raisi leo Jumapili amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Imam Ali Rahman wa Tajikistan huko Ashg-Abat mji mkuu wa Turkmenistan hiyo na kuongeza kuwa hakuna shaka kuwa uhusiano wa Tehran na Dushanbe utaendelea kustawi kwa sababu kiwango cha sasa cha ubadilishanaji wa kibishara kati ya pande mbili hakivutii. Amesema Iran na Tajikistan zinaweza kuimarisha kiwango cha uhusiano kati yazo kwa kuhuisha suhula za pande mbili.  

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Nchi mbili za Iran na Tajikistan zinapasa kushirikiana pakubwa na kwenda sambamba kifikra kuliko nchi nyingine kutokana na kuwa na uhusuano mkongwe wa kiutamaduni, kuwa na lugha moja, historia na urafiki wa muda mrefu baina yazo.  

Katika mazungumzo hayo waliyofanya hii leo huko Ashg-Abat, Rais Imam Ali Rahman wa Tajikistan ameashiria matukio ya karibuni huko Afghanistan na kusisitiza kuwa ukosefu wa amani unaoshuhudiwa nchini humo ni kwa madhara ya eneo na nchi jirani na Afghanistan; na pande zote zinapasa kufanya juhudi ili kaumu na makundi mbalimbali ya wananchi wa Afghanistan waishi kwa amani na utulivu. Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Iran yuko Ashg-Abat mji mkuu wa Turkimenistan kwa lengo la kushiriki Mkutano wa 15 wa Wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya ECO.  

Rais Raisi katika mazungumzo mjini Ashg-Abat na Rais Arif Alvi wa Pakistan

 

Tags