Nov 29, 2021 15:31 UTC
  • Mazungumzo ya Kamisheni ya Pamoja ya JCPOA yameanza leo Vienna Austria

Duru mpya ya mazungumzo ya Kamisheni ya Pamoja ya makubaliano ya nyuklia JCPOA imeanza leo katika mji mkuu wa Austria Vienna.

Ripoti zinasema kuwa, leo Novemba 29 mji mkuu wa Austria, Vienna ni mwenyeji wa mazungumzo baina ya Iran na nchi za kundi la 4+1 kuhusu kuondolewa vikwazo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya Iran.

Nchi zinaounda kundi la 4+1 ni China, Russia, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani pamoja na mwakilishi wa Umoja wa Ulaya. Mazungumzo hayo yameanza leo baada ya kusimama kwa takribani miezi mitano.

Ujumbe wa Iran katika mazungumzo hayo unaongozwa na Ali Baqeri, Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni anayeshughulikia masuala ya kisiasa ambaye aliwasili Vienna Jumamosi ya juzi akiongoza ujumbe wa  wataalamu wa masuala ya sheria, benki na nishati kwa ajili ya kushiriki katika mazungumzo hayo.

 

Ujumbe wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umefika katika meza ya mazungumzo huko Vienna kwa mujibu wa haki yake ya kisheria katika fremu ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kile inachotaka ni kuondolewa vikwazo vyote kwa njia ambayo itaweza kuthibitishwa kivitendo.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza mara kadhaa kwamba, lengo kuu la Tehran la kushiriki mazungumzo ya Vienna kuhusu mapatano ya nyuklia ya JCPOA yaliiyoanza leo ni kuhakikisha kuwa taifa hili linaondolewa vikwazo vyote haramu.

Tags