Nov 30, 2021 04:37 UTC
  • Tehran: Mazungumzo ya Vienna ni kwa ajili ya kuondolewa vikwazo ilivyowekewa Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, licha ya kwamba nchi za Magharibi zimeshindwa kutekeleza kabisa ahadi zao zote ndani ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA, lakini pamoja na hayo na kwa mara nyingine, Tehran imeamua kushiriki kwenye mazungumzo ili kuonesha nia yake njema na kufungua njia ya kuondolewa vikwazo vya kidhalimu ilivyowekewa Iran.

Hayo yalisemwa jana Jumatatu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdolahian na kuongeza kuwa, baada ya kufanyika mizunguko sita ya mazungumzo ya kina mjini Vienna, mazungumzo hayo yalishindwa kutokana na Marekani kujikumbizia kila kitu upande wake. 

Amesema hivi sasa tumeingia kwenye mzunguko mwingine wa mazungumzo hayo na lengo hasa ni kupigania haki za Iran na kuondolewa vikwazo vyote ambavyo viliwekwa na Marekani dhidi ya Tehran baada ya Washington kujitoa katika mapatano hayo. 

Pande za asili zilizofikia mapatano ya JCPOA kabla Marekani haijajitoa

 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa, tarehe 8 Mei, 2018, Marekani ilijitoa bila ya sababu katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA, hatua ambayo dunia nzima ilisema ni kinyume cha sheria. Dunia nzima inasema kwa kauli moja kwamba vitendo hivyo vya Marekani ni kinyume cha sheria, ni kudharau sheria za kimataifa, ni kutoheshimu hati ya Umoja wa Mataifa na ni katika njama za kuvuruga ushirikiano wa kimataifa kama ambavyo pia ni kuhatarasha amani na usalama wa dunia nzima.

Amesema, hatupaswi kusahau hata sekunde moja kwamba Marekani ndiyo iliyojitoa bila ya sababu katika mapatano ya nyuklia na ndiyo iliyopelekea kutokea hali iliiyopo hivi sasa katika makubaliano ya JCPOA.