Dec 17, 2021 08:04 UTC
  • Amir Abdolahian na mwenzake wa China wapongeza mwenendo wa mazungumzo ya Vienna

Hussein Amir Abdolahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran jana Alhamisi aliwasiliana kwa njia ya simu na na kufanya mazungumzo na mwenzake wa China, Wang Yi kuhusu uhusiano wa pande na kubadilishana mawazo juu ya mwenendo wa mazungumzo ya nyuklia ya Vienna na matukio ya kimataifa.

Katika mazungumzo hayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amepongeza msimamo wa  Beijing katika mazungumzo ya nyuklia ya Vienna na kusema mchakato wa mazungumzo hayo kiujumla ni mzuri. Wakati huo huo Abdolahian amekosoa kukosekana ubunifu wa pande za Magharibi huko Vienna.  

Mazungumzo ya kundi la 4+1 mjini Vienna Austria 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekosoa pia mienendo ya serikali ya Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi kuhusiana kususia kidiplomasia michezo ya Olimpiki ya Beijing ya msimu wa baridi na kueleza kuwa anataraji mashindano hayo yafanyika vizuri na kwa mafanikio. Ameongeza kuwa, viongozi wa ngazi ya juu wa michezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wataambatana na msafara wa wanamichezo wa Iran katika mashindano hayo. 

Katika mazungumzo hayo ya simu pande mbili zimesisitiza udharura wa kuendelezwa mashauriano na majadiliano ya kiufundi kati ya Tehran na Beijing kuhusu masuala ya nchi mbili na katika uga wa kimataifa.  

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa China ameutaja uhusiano wa nchi mbili kuwa ni wa kistratejia na kusema kuwa, serikali ya Beijing imeazimia kustawisha na kupanua uhusiano zaidi na Tehran.

Wakati huo huo Wang Yi ameunga mkono misimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kutilia mkao haja ya kushirikiana na nchi nyingine zinaoendelea duniani mkabala wa misimamo na hatua za upande mmoja na za kujitanua za madola makubwa duniani hususan Marekani. 

Tags