Jan 06, 2022 13:34 UTC
  • Wairani washiriki maziko ya mashahidi wao 250, Kiongozi Muadhamu atuma ujumbe

Wananchi wa Iran wamejitokeza kwa wingi katika maziko ya mashahidi wao 250 waliouawa wakati wa vita vya miaka minane vya kujihami kutakatifu vilivyoanzishwa na utawala wa kidikteta wa Saddam wa Iraq dhidi ya dola changa wakati huo la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Maziko hayo yamefanyika leo Alkhamisi sambamba na kumbukuku ya siku ya kufa shahidi Bibi Fatimatuz Zahra SA. 

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametuma ujumbe maalumu kwa mnasaba wa maziko ya mashahidi hao 250 yaliyofanyika katika kona zote za Iran na kuwaombea dua za kheri na kupandishwa daraja za juu za utukufu mbele ya Mwenyezi Mungu.

Kati ya mashahidi hao 250, ambao utambulisho wao haujulikani, wamo wale 150 waliozikwa katika mkoa wa Tehran na wengine 24 ambao maziko yao yamefanyika katika mikoa mingine ya Iran.

Kiongozi Muadhamu ametuma ujumbe maalumu kwa mnasaba wa maziko hayo

 

Mwaka 1980, dikteta wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein alianzisha mashambulizi ya pande zote kwa lengo la kuipindua Jamhuri ya Kiislamu ya Iran chini ya miaka miwili tu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu humu nchini. Saddam alianzisha uvamizi na mashambulio hayo kwa msaada wa madola makubwa ya Magharibi na vibaraka wao katika eneo hili. 

Hata hivyo wananchi mashujaa wa Iran wa matabaka yote walitii amri ya kiongozi wao, Imam Khomeini MA na kumiminika katika mistari ya mbele ya vita na kufanikiwa kuwatimua wanajeshi vamizi wa Iraq na kukomboa ardhi zao.

Vita hivyo vilimalizika mwaka 1988 kwa kufikiwa makubaliano ya kusimamisha vita huku dikteta Saddam Hussein akishindwa kufanikisha lengo lake lolote na hakuna hata shibri moja ya ardhi ya Iran iliyokuwa imebakia mikononi mwa adui mvamizi. 

Tags