Jan 08, 2022 12:32 UTC
  • Instagram yafuta jumbe zinazozungumzia Jenerali Soleimani

Wananchi wa Iran wameanzisha kampeni ya kulalamikia hatua ya mtandao wa kijamii wa Instagram ya kuendelea kufuta jumbe zinazohusiana na Luteni Jenerali Qasem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu wamekosoa vikali hatua ya shirika hilo la Kimarekani ya kufuta jumbe, picha, video na habari zinazohusiana na Shahidi Soleimani, ambaye alikuwa ni shujaa na nembo ya vita dhidi ya ugaidi katika eneo la Asia Mgharibi.

Afisa wa punde wa Iran kuathiriwa na kitendo hicho cha kubinya uhuru wa kujieleza ni Mohammad Medhi Esmaili, Waziri wa Utamaduni wa Iran, ambaye alikuwa ametuma ujumbe kwa mnasaba wa mwaka wa pili wa mauaji ya kigaidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani mjini Baghdad.

Katika hali ambayo mashirika ya mitandao ya kijamii Marekani huwapa jukwaa wale wenye chuki dhidi ya Uislamu na Iran kwa kisingizio cha ‘uhuru wa maoni’ lakini kitendo chao cha kukanyaga uhuru huo ni ishara ya wazi ya undumakuwili wa dola hilo la kibeberu.

Shahidi Soleimani ambaye Januari 3 mwaka 2020 alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha'abi na wanajihadi wengine wanane katika shambulio la kigaidi la jeshi la kigaidi la Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad. 

Hujuma hiyo ya kinyama ilitekelezwa kufuatia amri ya rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump, ambaye alijitokeza hadharani na kukiri waziwazi kuhusu jinai hiyo, ambayo ni mfano wa wazi wa ugaidi wa kiseriali wa Washington.

Tags