Jan 10, 2022 08:51 UTC
  • Khatibzadeh: Ipo ajenda ya kufanyika duru ya tano ya mazungumzo baina ya Iran na Saudia

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran amesema Iran na Saudia zinapanga kufanya awamu ya tano ya mazungumzo chini ya uenyeji wa nchi ya Iraq.

Saeed Khatibzadeh ambaye alikuwa akizungumza na waandishi habari leo Jumatatu kuhusu awamu ya tano ya mazungumzo baina ya Iran na Saudi Arabia na kwamba je misimamo ya Riyadh kuhusu Lebanon na Hizbullah itaathiri mazungumzo hayo au la, amesema duru ya tano ya mazungumzo ya Tehran na Riyadh itafanyika chini ya uenyekiti wa Iraq na kwamba mazungumzo hayo yataendelea kwa kuzingatia maslahi na uwazi licha ya mafaili kadhaa ya hitilafu baina ya pande mbili.

Kuhusu uingiliaji wa nchi za kigeni katika masuala ya ndani ya Lebanon, Khatibzadeh amesema, nchi zote zinapaswa kuheshimu mamlaka ya kujitawala ya mataifa mbalimbali. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria pia safari ya ujumbe wa Taliban mjini Tehran na kusema: Hali ya sasa ya Afghanistan inaitia wasiwasi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwamba safari ya saa ya maafisa wa Taliban inafanyika katika mkondo huo.   

Tags