Jan 14, 2022 12:21 UTC
  • Raisi: Vikwazo na vitisho haviwezi kulizuia taifa kustawi na kupata maendeleo

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, vikwazo na vitisho kamwe haviwezi kulizuia taifa la Iran kustawi na kupata maendeleo.

Rais Ebrahim Raisi amesema hayo leo Ijumaa katika siku ya pili ya safari yake ya kutembelea mkoa wa Hormozgan wa kusini mwa Iran. 

Wakati akikagua maonyesho ya maendeleo na mafanikio ya Kikosi cha Majini cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, Rais Raisi amesema, licha ya kuweko vikwazo vya kila upande dhidi ya Iran hasa vya kijeshi na vya mradi wa nyuklia, lakini taifa hili la Kiislamu limepiga hatua kubwa katika nyuga za kiulinzi na teknolojia ya nyuklia.

Baadhi ya boti zenye kasi kubwa za Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH

 

Amesisitiza kuwa, maadamu moyo huu wa kimapinduzi na wa kujitolea utaendelea kuwepo, kamwe adui hatoweza kulifanya chochote taifa kubwa la Iran.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia amesema, leo hii wananchi wa Iran hawana wasiwasi wowote kuhusu usalama wa nchi yao katika pembe zake zote kwani hakuna harakati yoyote ya adui ambayo inaweza kufumbiwa macho na walinzi mashujaa wa taifa hili.

Rais Ebrahim Raisi aliwasili mkoani Homozgan (Hormozgan) Jumatano ikiwa ni safari yake ya 14 ya kutembelea mikoa mbalimbali ya Iran tangu awe Rais wa Jamhuri ya Kiislamu. Anafanya ziara hizo za kikazi ili kuonana kwa karibu na wananchi na kutatua yeye mwenyewe matatizo hata ya watu wa chini kabisa.

Tags