Jan 17, 2022 08:03 UTC
  • Benki ya Dunia:  Uchumi wa Iran ulistawi kwa asilimia 3.1 mwaka 2021

Benki ya Dunia imesema uchumi wa Iran ulistawi kwa asilimia 3.1 mwaka 2021 na hivyo kupiga hatua zaidi ya utabiri wa benki hiyo ambayo ilikuwa imetabiri Juni mwaka jana kuwa ustawi huo ungekuwa kwa asilimia moja.

Taarifa ya Jumapili ya Benki ya Dunia kuhusu 'Makadirio ya Ustawi wa Uchumi wa Dunia' inaonyesha kuwa Jumla ya Pato la Taifa (GDP) la Iran lilifika asilimia 3.1 mwaka 2021 na hivyo uchumi wa nchi hii umeweza kustawi kwa kasi zaidi ya ilivyotabiriwa. Aidha GDP ya Iran mwaka 2020 ilikuwa ni 3.4 baada ya uchumi kudorora kwa asilimia 6.8 mwaka 2019 kutokana na vikwazo vya kidhalimu vya Marekani ambavyo vilizuia nchi hii kuuza nje mafuta ghafi ya petroli.

Ustawi wa uchumi wa Iran kwa muda wa miaka miwili mfululizo unajiri pamoja na kuwa Marekani ilishadidisha vikwazo vyake mwaka jana wakati nchi hii ikiwa katikati ya vita dhidi ya maambukizi ya COVID-19.

Tawkimu za Benki ya Dunia zinathibitisha ukweli katika kauli ya wakuu wa Iran ambao wanasema kuwa nchi hii imeweza kuvuka athari mbaya za vikwazo vya Marekani na janga la COVID-19.

Kituo cha kusafisha mafuta

Ripoti hiyo ya Benki ya Dunia inaonyesha kuwa mwaka jana GPD ya Iran ilikuwa juu zaidi ya Saudi Arabia ambayo ni muitifaki mkubwa wa Marekani. Benki ya Dunia imebaini kuwa GDP ya Saudi Arabia, muuzaji mkubwa zaidi ya mafuta duniani, ilistawi kwa asilimi 2.4 mwaka 2021.

Aidha ripoti hiyo ya Benki ya Dunia imetabiri kuwa, katika mwaka huu wa 2022, uchumi wa Iran utastawi kwa asilimia 2.4

 

Tags