Jan 18, 2022 08:08 UTC
  • Kuanza kupelekwa barani Ulaya huduma za nishati za Iran

Kufuatia kutiwa saini hati ya mapatano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Romania kwa ajili ya kupelekwa nchini humo huduma za kiufundi za Iran katika sekta ya gesi, kwa mara ya kwanza Iran imejiunga na nchi zinazouza barani Ulaya huduma za nishati.

Kwa mujibu wa mapatano hayo, sasa Iran itaanza kutekeleza nchini Romania miradi mikubwa ya kutoa huduma za kiufundi katika nyanja za kusambaza gesi na kujenga vituo vya kuhifadhi gesi katika nchi hiyo ya Ulaya.

Hayo ni kwa mujibu wa mapatano yaliyofikiwa karibuni kati ya Shirika la Uhandisi na Ustawi wa Gesi la Iran na Shirika la Gaz Vest la Romania.

Kama alivyosema Reza Noushadi, mkurugenzi mkuu mtendaji wa shirika la huduma za kiufundi nchini Iran, lengo la kutiwa saini mapatano hayo ni kuchunguzwa fursa za uwekezaji wa pamoja na ushirikiano katika nyanja tofauti za nishati ya gesi.

Mtambo wa kuchimba gesi baharini

Kwa kuwa na mtandao mkubwa wa mabomba ya kusafirishia gesi yenye urefu wa maelfu ya kilomita na vituo vingine muhimu vya nishati ya gesi, Iran ni moja ya nchi zilizo na uzoefu mkubwa katika uwanja huo na inatengeneza ndani ya nchi vifaa vingi vinavyohitajika katika utekelezaji wa miradi muhimu katika sekta hiyo.

Tags