Jan 23, 2022 08:14 UTC
  • Spika Qalibaf: Sera za nje za serikali ya 13 zimefungua dirisha jipya kwa ajili ya kudhamini maslahi ya taifa

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema, sera za nje za serikali ya 13 zimefungua dirisha jipya kwa ajili ya kudhamini maslahi ya taifa.

Mohammad Baqer Qalibaf ameyasema hayo mapema leo katika hotuba ya kabla ya kikao cha bunge, ambapo sambamba na kutoa mkono wa heri, baraka na fanaka kwa mnasaba wa maadhimisho ya kuzaliwa Bibi Fatimatu-Zahra (AS) na Siku ya Mwanamke, ameeleza kuwa, muelekeo wa serikali ya 13 wa kuzingatia uhalisia wa mambo na mashirikiano ya kambi kadhaa ili kuweza kunufaika na fursa zote za kistratejia za Iran katika uga wa sera za nje, umefungua dirisha jipya kwa ajili ya kudhamini maslahi ya taifa hasa katika kufaidika na fursa za kiuchumi zilizoko nchini.

Bunge la Iran

Spika wa Bunge la Iran ameongeza kuwa, leo hii kuwa na uhusiano wa nje wenye mlingano, unaozingatia kujitawala, heshima ya taifa, diplomasia ya kuzingatia uhalisia wa mambo, na ufahamu unaotilia maanani uhakika kuhusu mfumo wa kambi kadhaa unaotawala katika mahusiano ya kimataifa, ni udharura usioweza kukanushika.../