Jan 23, 2022 12:21 UTC
  • Kiongozi Muadhamu awataka wasomaji wa tungo za kuwasifu Ahlul-Beiti (as) kukabiliana na propaganda dhidi ya Iran

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewataka wasomaji wa tungo za mashairi ya kuwasifu Ahlul-Beiti (as) kutumia nafasi waliyonayo kwa ajili ya kukabiliana na propaganda za vyombo vya habari dhidi ya taifa la Iran.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, amesema hhayo leo mbele ya hadhara ya wasomaji wa tungo za kuwasifu Ahlul-Beiti wa Mtume (saw) kwa mnasaba wa maadhimisho ya kuzaliwa Bibi Fatima (as), binti ya Mtume Mtukufu (saw).

Kiongozi Muadhamu ameashiria baadhi ya sifaa aali za shakhsia ya Bibi Fatma Zahra (as) na kubainisha kwamba, nafasi na daraja ya utoharifu, kufanya kazi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kuhudumia pasi na masimbulizi na nafasi bora katika kukabiliana na kambi ya batili katika kadhia ya Mubahala (kuapizana) ni miongoni mwa sifa zisizo na mithili za bibi mwema huyo na mtoharifu ambazo zimeashiriwa wazi katika Qur'ani.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, jamii ya Iran imekuwa mfuasi wa mwenendo wa Bibi Fatma na katika kipindi chote cha miaka 43 kumeshuhudiwa mara chungu nzima harakati zenye kufuata mwenendo wa Bibi Fatma iwe ni katika kipindi cha kujihami kutakatifu, katika harakati ya kielimu au katika utoaji huduma usio na masimbulizi. 

 

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, ulimwengu mzima hususan harakati za kijamii na kimapinduzi zinapaswa kumfanya Bibi Fatma Zahra (as) kuwa riwaza na kigezo chao.

Kiongozi Muadhamu ameashiria hujuma na njama kubwa za maadui wa taifa la Iran zenye lengo la kuzipotosha fikra za wananchi wa Iran na kuhharibu imani na itikadi zao kupitia propaganda za vyombo vya habari na  na kubainisha kwamba, medani muhimu ya jihadi ni kubainisha na kuweka wazi mambo.