Jan 26, 2022 04:15 UTC
  • Rais wa Iran: Endapo vikwazo vya kidhalimu vitaondolewa kuna uwezekano wa kufikiwa makubaliano

Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, endapo pande husika katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA zitakuwa tayari kuliondolea vikwazo vya kidhalimu taifa hili, basi kuna uwezekano wa kufikiwa aina yoyote ya makubaliano kamili.

Sayyid Ebrahim Raisi amesema hayo alipozungumza na taifa kupitia televisheni ambapo amebainisha kwamba, matokeo ya safari na mazungumzo na viongozi wa mataifa mbalimbali yanapaswa kudhamini maslahi ya taifa hili, kupanuliwa wigo wa ustawi katika nyanja mbalimbali na kwamba, kutoa tabasamu tu bila ya kuweko matunda na matokeo ni jambo lisilo na faida yoyote kwa wananchi.

Rais Ebrahim Raisi amesisitiza kuwa, kama katika mazungumzo yanayoendelea hivi sasa huko Vienna Austria pande husika zitakuwa tayari kuliondolea vikwazo vya kidhalimu dhidi ya taifa la Iran, basi kuna mazingira na uwanja wa kufikiwa makubaliano.

Rais Ibrahim Rais katika akiwa katika mahojiano na wanahabari wa Kanali ya Sita ya Habari ya Jamahuri ya Kiislamu ya Iran

 

Akijibu swali kuhusiana na jinsi mazungumzo ya Vienna yanayoendelea na kwamba, msimamo wa Iran ni upi ikiwa Marekani itataka kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na taifa hili, Rais Ebrahim Raisi amesema, kwa muda sasa Washington imekuwa ikitoa ombi hilo lakini hadi sasa mazungumzo hayo hayajafanyika.

Aidha amesema, serikali ya sasa inalenga kuwa na ushirikiano na dunia nzima na kuongeza kwamba, serikali ya awamu ya 13 inafuatilia suala la kuwa na uhusiano na mataiifa yote ya dunia yanayotaka kuwa na uushirikiano na Tehran. Hata hivyo Rais wa Iran ameonya kwamba, kama mataifa ya dunia yatataka kukabiliana na Iran basi Tehran nayo itasimama kukabiliana nayo.

Tags