Mar 05, 2022 14:22 UTC

Kamanda wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh amesema Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yameimarisha mara saba zaidi uwezo wa makombora na kuvurmisha makombora mengi kwa wakati moja na pia uwezo wa ndege za kivita zisizo na rubani au drone.

Ameyasema hayo  leo wakati wa kuzindiliwa vituo viwili vipya vya makombora na ndege za kivita zisizo na rubani  vya Kikosi cha Anga cha IRGC katika sherehe ambayo pia imehudhuriwa na kamanda mkuu wa IRGC.

Vituo hivyo viwili vya kijeshi vimejengwa katika kina cha milima chenye njia za chini kwa chini za makombora ya nchi kavu kwa nchi kavu na pia ndege za kivita zisizo na rubani au drone ambazo zinaweza kujipenyeza katika ngome za maadui bila kuonekana katika rada. Amesema vituo hivyo vipya vya kijeshi vinasimamiwa na vijana wanamapinduzi na vitakuwa ngome imara ya Iran ya Kiislamu katika kukabiliana na maadui wa nchi hii.

Hii ni mara ya kwanza kwa IRGC kuzindua kituo cha ndege za kivita zisizo na rubani kilicho katika kina cha milima.

Ndege za kivita zisizo na rubani za IRGC zikiwa katika kituo kipya kilichojengwa chini ya ardhi katika milima

Brigedia Jenerali Hajizadeh amesema muda wa kutayarisha na kuvurumisha makombora yaliyo katika eneo hilo la siri ni mfupi sana. Aidha amesema kituo hicho kina uwezo wa kubeba drone sitini ambazo zinaweza kutumiwa eneo lolote lile.

Akizingumza katika hafla hiyo, Kamanda Mkuu wa IRGC Meja Jenerali Hossein Salami amesema Iran haitegemei silaha bali kile inachotegemea ni azma, irada na imani ya wananchi lakini akaongeza kuwa Iran hivi sasa ina silaha za kutosha ambazo zimeundwa kwa kutegemea uwezo wa wataalamu wa ndani ya nchi.

Tags