Apr 14, 2022 07:01 UTC
  • Zahra Ershadi
    Zahra Ershadi

Zahra Ershadi, balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa: "Kuzikalia kwa mabavu ardhi za mataifa mengine, uvamizi wa kigeni na ugaidi ndio vitisho vikuu kwa usalama wa wanawake katika Asia Magharibi."

Zahra Ershadi, ambaye alikua akihutubia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake, amani na usalama kilichofanyika jana ameashiria hali ya wanawake katika eneo la Magharibi mwa Asia, ikiwemo Palestina na kusema: "Unyanyasaji wa kingono ni uhalifu wa kutisha ambao mara nyingi hutumika kama mbinu ya vita na ugaidi.

Amesema vitisho vikuu kwa usalama wa wanawake katika eneo la Asia Magharibi ni pamoja na uvamizi wa kigeni na ugaidi, na kwamba vitisho hivyo haviheshimu haki na maisha ya wanawake. Amesema, hali ya wasichana na wanawake wa Kipalestina ni mfano wa wazi wa ukweli huo.

Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema "Katika migogoro ya silaha, unyanyasaji wa kingono huathiri kwa kiasi kikubwa wanawake na wasichana pamoja na watu walio katika mazingira magumu, na kusisitiza kuwa wanawake na wasichana ndio waathirika wakuu.

Wanawake waliokuwa wametekwa nyara ya kundi la kigaidi la Boko Haram, Nigeria

Ershadi ameongeza kuwa, migogoro ya silaha pia huzidisha hatari ya magendo ya binadamu, ambayo inawalenga zaidi wanawake na watoto wanaokimbia vita au kuhamishwa kwa nguvu.

Ershadi amesisitiza kuwa kuzuia na kupambana na vitendo hivyo visivyo vya kibinadamu kunahitaji juhudi za pamoja na kusema: “Hata hivyo, jitihada hizo hazitafanikiwa hadi pale sababu kuu, yaani mazingira ya kuzuka kwa vita vya kutumia silaha, zitakapopatiwa ufumbuzi na kutatuliwa.”

Tags