Apr 22, 2022 07:11 UTC
  • Al-Jazeera: Iran imeionya Israel, yaiambia maghala yako ya silaha yatalengwa

Televisheni ya Al-Jazeera ya Qatari imeripoti kuwa, Iran imetuma picha na ramani za maghala ya silaha za nyuklia za utawala wa Kizayuni kwa serikali ya Tel Aviv kupitia nchi moja ya Ulaya.

Shirika la habari la Iran Press lmenukuu ripoti ya Al-Jazeera ya Qatar ikitangaza habari hii ikinukuu chanzo cha Iran ambacho hakikutajwa kwa jina.

Al Jazeera pia imesema, nyingi kati ya ramani na picha hizo zilichukuliwa kutoka ardhini na hazikuwa picha za satelaiti.

Pia iliwekwa alama nyekundu kwenye kuta za maeneo ya kuhifadhia silaha ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya Aljazeera, Iran imeuonya utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba iwapo utathubutu kuishambulia Iran, maghala hayo na silaha yatakuwa shabaha halali ya Jamhuri ya Kiislamu.

Al-Jazeera pia imeripoti kuwa, hapo awali Israel ilibadilisha eneo la maghala yake za silaha za kistratijia, na kwamba picha hizo mpya zilizotumwa na Iran kwa viongozi wa utawala huo ghasibu kwa hakika zinahusiana na maghala mapya ya silaha za kistratijia ya utawala huo.

Siku chache zilizopita Rais wa Jamhri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Ebrahim Raisi alisema kuwa, uchokozi hata mdogo zaidi wa maadui kama vile utawala wa Kizayuni wa Israel hautafumbiwa macho na vikosi vya ulinzi vya Iran.

Rais Ebrahim Raisi

Rais Ebrahim Raisi ameyasema hayo leo mjini Tehran alipohutubu kwa mnasaba wa Siku ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Rais Raisi aliuonya vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kusema: "Isarel inafahamu kwamba harakati yake ndogo zaidi inafuatiliwa kwa karibu na majeshi yetu. Wakifanya kosa lolote, majeshi yetu yatafika katika kitovu cha utawala wa Kizayuni na uwezo wa majeshi yetu hautawaacha katika utulivu."

Tags