May 01, 2022 11:21 UTC
  • SEPAH: Madola ya kigeni ndilo tishio la usalama wa Asia Magharibi

Kamanda wa Kikosi cha Majini cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesisitiza kuwa madola ya kigeni yaliyojizatiti na majeshi yao kwenye eneo hili, ndilo tishio kwa usalama wa Asia Magharibi.

Nahodha Alireza Tangsiri amesema hayo na kuongeza kuwa, nchi za eneo hili zinaweza kujilinda na kujidhaminia zenyewe usalama wao na hazina haja na madola baki ambayo hayalipendelei kheri hata kidogo eneo hili. 

Kamanda Tangsiri pia amesema, mara kwa mara Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikutuma ujumbe wa amani na urafiki kwa nchi majirani zake zikiwemo zinazopakana na Ghuba ya Uajemi ikisisitiza kuwa, kwa kushirikiana pamoja tunaweza kulinda usalama wetu na hatuwahitajii kabisa wageni. Amesema, si tu madola hayo ajinabi hayalipendelei kheri eneo hili, lakini pia ndiyo yanayohatarisha usalama wa nchi za ukanda huu mzima ili kupata kisingizio cha kuendelea kubakia kinyume cha sheria katika eneo nyeti na muhimu sana la Asia Magharibi.

Wanajeshi magaidi wa Marekani baada ya kutiwa mbaroni na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH

 

Kamanda wa Kikosi cha Majini cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesisitiza pia kuwa, Marekani na nchi nyingine kutoka nje ya eneo hili, hazikuwa na nafasi yoyote kwenye ukanda huu na kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel nao kamwe hauwezi kuwa na nafasi katika eneo hili. 

Pia amesema, Iran imeweza kuvulimia kwa kiwango fulani lakini kama subira yake itaisha, bila ya shaka yoyote itatoa majibu ya haraka na papo hapo dhidi ya nchi yoyote itakayohatarisha manufaa yake katika eneo la Ghuba ya Uajemi.

Kamanda Tangsiri aidha amesema, jina la Ghuba ya Uajemi ni muhimu sana akisisitiza kuwa hapa ni Ghuba ya Uajemi na hakuna yeyote anayeweza kubadilisha jina hilo na kupandikiza jina bandia.

Tags