May 15, 2022 12:09 UTC
  • Bagheri Kani: Siasa za kiistratijia za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kufelisha vikwazo

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, siasa za kimkakati za Jamhuri ya Kiislamu ni kufelishi vikwazo.

Shirika la habari la Iran Press limemnukuu Ali Bagheri Kani ambaye pia ni mkuu wa timu ya Iran ya mazungumzo ya nyuklia huko Vienna Austria akisema hayo na kusisitiza kuwa, siasa za kiistratijia za Jamhuri ya Kiislamu ni kufelisha vikwazo wakati sambamba na kufanya ubunifu wa kiakili na kibusara ili kupambana na vikwazo hivyo na kuhakikisha kuwa njama zoe za adui za kujaribu kukwamisha maendeleo ya pande zote ya Iran, zinashindwa kikailifu.

Amesema, hivi sasa nchi nyingine zilizokumbwa na vikwazo zinaiomba Iran izipe utaalamu wa kufelisha vikwazo zinavyowekewa.

Ali Bagheri Kani

 

Awamu ya nane ya mazungumzo ya uondoaji vikwazo ilianza mjini Vienna, tarehe 27 D1semba 2021; na baada ya kusitishwa kwa kipindi kifupi ili pande husika ziende kufanya mashauriano katika miji yao mikuu, ilianza tena tarehe 8 Februari, katika mji mkuu huo wa Austria.

Sasa hivi mazungumzo hayo yamesitishwa tena kwa pendekezo la Josep Borrell, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya; ambapo timu za mazungumzo zimerejea tena katika miji yao mikuu kwa mashauriano zaidi. 

Kwa upande wake, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema mazungumzo ya Vienna yamefika awamu ambayo fundo hilo linaweza kufunguliwa iwapo tu upande uliokiuka makubaliano ya JCPOA hasa Marekani utashehimu njia za ufumbuzi wa kimantiki na kwa mujibu wa sheria.

Tags