May 17, 2022 03:04 UTC
  • Khatibzadeh: Marekani inapaswa kuchukua maamuzi ya kisiasa

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria safari ya mratibu wa mazungumzo ya nyuklia ya Vienna, ubunifu na mapendekezo maalumu ya Iran na kusema kuwa, Marekani inapaswa kuchukua maamuzi ya kisiasa.

Saeed Khatibzadeh amesema hayo katika mkutano wake wa kila wiki na waandishi wa habari hapa mjini Tehran na kubainisha kwamba, katika safari ya hivi karibuni hapa Tehran ya Enrique Mora, mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya anayehusika na uratibu wa mazungumzo ya nyuklia ya Vienna kulipatiwa ufumbuzi baadhi ya mambo na kutolewa mapendekezo na ikaamuliwa kuwa, kama Marekani itatoa majibu kwa mapendekezo hayo basi Iran nayo itakuwa katika nafasi ya pande zote kurejea katikak mazungumzo ya Vienna kwa ajili ya maafikiano.

 

Hivi majuzi pia, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisisitiza kwamba, kilichobakia kuhusu mazungumzo ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA ni maamuzi ya kisiasa tu, na kama wanasiasa watachukua maamuzi sahihi, basi mazungumzo hayo yatakamilika.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia harakati za utawala ghasibu wa Israel na kueleza kwamba, kila mara kunapofanyika ubunifu katikak uga wa diplomasia utawala bandia unaoikalia kwa mabaavu Quds nao huchukua hatua za jaddi dhidi ya diplomasia na kwa hakika jambo hilo siyo geni.