May 18, 2022 14:29 UTC
  • Ripota maalumu wa UN: Marekani isimamishe vikwazo vyote vya upande mmoja dhidi ya Iran

Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa anayefuatilia taathira hasi za hatua za upande mmoja kwa haki za binadamu ameitaka Marekani isimamishe vikwazo vyote vya upande mmoja ilivyoiwekea Iran na kusisitiza kuwa kuiwekea vikwazo Iran ni ukiukaji wa haki za binadamu.

Katika miongo ya karibuni vikwazo vya kiuchumi vimegeuzwa na nchi zinazotumia mabavu kuwa wenzo wa kuzishinikiza nchi zenye sera na misimamo huru katika uga wa kimataifa. Kuanzia muongo wa 1990, Marekani, Umoja wa Ulaya na madola mengine yaliyostawi kiuchumi yamechukua mara mia kadhaa hatua za kuziwekea vikwazo vya kiuchumi nchi zingine.

Tangu Mapinduzi ya Kiislamu yalipopata ushindi, maadui wa wananchi wa Iran wamekuwa kila mara wakiliwekea taifa hili vikwazo vya kidhalimu kwa madhumuni ya kuudhuru uchumi wake na hawajasita kuiwekea vikwazo sekta yoyote ile ya Iran.

Kutokana na hatua hizo za kidhalimu, Profesa Alen Douhan, ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa anayefuatilia taathira hasi za hatua za upande mmoja kwa haki za binadamu, ambaye amefanya ziara hapa mjini Tehran amezitaka nchi zote zilizoiwekea vikwazo Iran na hasa Marekani zisimamishe vikwazo ilivyowawekea watu wa taifa hili katika nyanja za chakula, dawa, maji na afya.

Douhan ameongeza kwa kusema "serikali ya Marekani iziachie mali zote za Benki Kuu ya Iran ilizozizuia; na kwa ajili ya haki za binadamu, ninayataka mabenki yote na mashirika yote ya binafsi yasikubali kutekeleza vikwazo hivi".../