May 19, 2022 02:26 UTC
  • Mokhber: Uhusiano wa Iran na nchi za Afrika umeingia mkondo mpya

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ushirikiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi za Afrika ikiwemo Ghana umechukua mkondo mpya.

Mohammad Mokhber Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran ameyasema hayo Jumatano mjini Tehran alipokutana na kufanya mazungumzo na Ibrahim Mohammed Awal, Waziri wa Ghana wa Utamaduni, Sanaa na Utamaduni. Katika kikao hicho, Mokhberi amesisitiza kuwa, serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina hamu na motisha ya juu katika kuimarisha na kuboresha uhusiano na Ghana. Aidha amesema uhusiano wa kibiashara na kichumi baina ya Iran na Ghana unapaswa kupanuka zaidi kama ulivyo uhusiano wa kisiasa.

Halikadhalika ameashiria huduma na misaada ya kiafya ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa watu wa Ghana hasa kupitia Hilali Nyekundu ya Iran nchini  humo na kusema: "Iran iko tayari kuwa na ushurikiano zaidi na Ghana katika sekta za kilimo nje ya mipaka, huduma ufundi na uhandisi na uwekezaji katika sketa binafsi ya nchi."

Mohammad Mokhber Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran akiamkuana na Ibrahim Mohammed Awal, Waziri wa Ghana wa Utamaduni, Sanaa na Utamaduni.

 

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aidha ameashiria nafasi ya Ghana katika kustawisha amani na duniani hasa kupitia Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote. 

Kwa upande wake, Ibrahim Mohammed Awal, Waziri wa Ghana wa Utamaduni, Sanaa na Utalii amesisitiza kuhusu kuimarishwa kiwango cha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara baina ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Ghana na kusema nchi yake itatumia uwezo wake  wote kuimarisha uhusiano huo.

Ibrahim Mohammed Awal ambaye pia ni mwenyekiti wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano wa Iran na Ghana amesema serikali ya Ghana inaunga mkono shughuli za kiuchumi na kibiashara za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Ghana.

Tags