May 23, 2022 09:44 UTC
  • SEPAH: Maadui wamedhihirisha tena dhati ya shari yao kwa kumuua shahidi Sayyad Khodaei

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) limelaani mauaji ya mmoja wa askari wake ambaye ni mlinzi wa Haram na kueleza kwamba, maadui kwa mara nyingine tena wamedhihirisha dhati ya shari yao kwa ugaidi.

Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) amesisitiza kuwa, makundi ya kigaidi yenye mfungamano na uistikbari na Uzayuni wa kimataifa yanalipa gharama kwa jinai zao.

Brigedia Jenerali Ramezan Sharif, msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) ameeleza kuwa, kuuawa shahidi Kanali Hassan Sayyad Khodaei kutaongeza azma ya jeshi la SEPAH ya kulinda usalama, mamlaka ya kujitawala na maslahi ya kitaifa sambamba na kukabiliana na maadui wa taifa la Iran.

Idara ya Mahusiano ya Umma ya SEPAH jana ilitangaza kuwa mmoja wa askari wake ambaye ni Mlinzi wa Haram ameuawa shahidi katika hujuma ya kigaidi mjini Tehran Jumapili jioni.

Brigedia Jenerali Ramezan Sharif, msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH)

 

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la SEPAH, askari mwenye kuheshimika mlinzi wa Haram Kanali Hassan Sayyad Khodaei aliuawa shahidi katika hujuma ya kigaidi ya wapinga Mapinduzi ya Kiislamu na maajenti wa madola ya kiistikbari duniani.

Katika taarifa Jumapili usiku, Saeed Khatibzadeh, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alituma salamu za pongezi na rambirambi kwa familia ya Shahidi Sayyad Khodaie.

Kufuatia jinai hiyo, Jaji wa Mahakama ya Uadilifu Tehran, Ali Alqasi amemuamuru Mwendesha Mashtaka wa Tehran achukue hatua za haraka za kuwakamata waliohusika na jinai hiyo.

Tags