May 24, 2022 08:18 UTC
  • Spika: Mauaji ya Shahidi Khodaei yameweka wazi zaidi woga na ushenzi wa utawala wa Kizayuni

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema tukio la kigaidi la mauaji ya Mlinzi wa Haram Shahidi Hassan Sayyad Khodaei kwa mara nyingine tena limeweka wazi zaidi sura iliyojaa woga na ukatili ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Sambamba na kutoa mkono wa pongezi na pole kwa kuuawa shahidi Hassan Sayyad Khodaei kwa Imam wa Zama (AS), Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, wananchi wa Iran, wapiganaji wenzake Shahidi Khodaei pamoja na familia yake azizi, Mohammad Baqir Qalibaf amesema: tukio la kigaidi la mauaji ya Mlinzi wa Haram Shahidi Hassan Sayyad Khodaei kwa mara nyingine tena limeweka wazi zaidi sura iliyojaa woga na ukatili ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Qalibaf ameongeza kuwa maadui wenye nyoyo zilizopofuka, ambao wameshindwa kukabiliana na moyo wa subira, muqawama na moyo wa kujitolea wa taifa la Iran wameamua kuchukua hatua za aina hiyo dhalili na zilizo nje ya vipimo vya kimataifa na kiutu, ambazo bila shaka hazitakuwa na faida yoyote kwao.

Kushoto: Shahidi Hassan Sayyad Khodaei. Kulia: eneo la tukio aliposhambuliwa ndani ya gari mbele ya nyumba yake

Spika wa Bunege la Iran ameendelea kueleza kuwa baada ya miaka kadhaa ya jihadi katika njia ya kufanikisha malengo matukufu ya Mapinduzi, thamani za Kiislamu na sha'ari za AhluBaiti (AS), Shahidi mwenye daraja ya juu Hassan Sayyad Khodaei ameifikia hadhi ya kufa shahidii ili kuthibitika kuwa, kama ilivyo kila siku zote watoto wa taifa shujaa la Iran wataendelea kwa heshima na ushujaa kushikamana na malengo na mapiganio matukufu ya kukabiliana na Uistikbari na utawala khabithi wa Kizayuni.

Halikadhalika amesisitiza ulazima wa vyombo vya usalama na intelijensia kuchukua hatua za lazima za kuwatambua na kuwaadhibu waliohusika katika utekelezaji na walioamuru kutekelezwa hujuma hiyo ya kigaidi.

Kanali Hassan Sayyad Khodaei aliuawa shahidi siku ya Jumapili kwa kupigwa risasi tano na mamluki magaidi wa Uistikbari wa dunia katika mtaa wa Mojahidina Eslam mjini Tehran.../

Tags