May 27, 2022 11:10 UTC
  • Hujjatul Islam Kazem Seddiqi : Muqawama wa Lebanon ulivunja pembe ya Wamarekani

Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran ametoa pongezi kwa mnasaba wa maadhimisho ya miaka 22 ya ushindi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon dhidi Wazayuni na kusema, Wazayuni walionja ladha chungu ya kwanza ya kushindwa baada ya kuondoka kwa madhila huko kusini mwa Lebanon.

Hujatul-Islam Wal-Muslimin Hujjatul Islam wal Muslimin Kazem Seddiqi  ameyasema hayo katika hotuba za ibada ya kisiasa na kimaanawi ya Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran na kubainisha kwamba, kushindwa kwa madhila Wazayuni kusini mwa Lebanon miaka 22 iliyopita kulivunja pembe ya Wamarekani.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran ametoa mkono wa kheri na pongezi kwa mnasaba huu kwa Sayyid Hassan Nasrullah kamanda shupavu wa muqawama na wananchi wa Lebanon pamoja na kambi ya muqawama kwa ujumla.

Itakumbukuwa kuwa, tarehe 25 Mei 2000, utawala wa Kizayuni wa Israel licha ya kuwa na nguvu za kijeshi, ulisalimu amri mbele ya wanamapambano wa Kiislamu wa Lebanon na ulilazimika kukimbia kwa madhila kutoka kusini mwa nchi hiyo.

 

Kila mwaka wananchi wa Lebanon wanaadhimisha siku hiyo ya kukimbia wanajeshi wa mwisho wa Israel kusini mwa nchi yao na siku hiyo wanaiita "Siku ya Muqawama na Ushindi."

Katika sehemu nyingine ya hotuba zake katika Swala ya Ijumaa mjini Tehran, Hujjatul Islam wal Muslimin Kazem Seddiqi amesema, Saudi Arabia iligharanmika pakubwa katika uchaguzi wa hivi karibuni wa Bunge nchini Lebanon ikiwaunga mkono wanasiasa ambao ni vibaraka wa Marekani, hata hivyo imeshindwa vibaya na licha propaganda zote, lakini wagombea wanaoungwa mkono na Hizbullah na muqawama ndio walioibuka na ushindi.

Tags