Jun 23, 2022 08:03 UTC
  • Raisi asisitiza: Ni marufuku kuwepo kivyovyote na kuingilia nchi ajinabi katika bahari ya Kaspi

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuhusu umuhimu wa kushirikiana nchi majirani katika eneo la Kaspi na kupigwa marufuku uwepo wowote wa wanajeshi ajinabi katika eneo hilo hasa katika mazingira maalumu ya eneo la Pwani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ambaye jana Jumatano aliwasili hapa Tehran kwa mwaliko wa waziri mwenzake wa Iran Amir Abdullahian amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Iran. 

Amir Abdullahian na Sergei Lavrov hapa Tehran 

Rais Ebrahim Raisi jana usiku alikuwa na mazungumzo na Sergei Lavrov ambao alisema, mazungumzo endelevu baina ya Russia na viongozi wa Iran yanashiria irada thabiti ya nchi mbili ya kuanza kipindi kipya cha ushirikiano wa kistratejia kwa manufaa ya watu wa nchi mbili ikiwemo pia kushirikiana katika sekta ya uchumi.  

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema baada Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia kuwasilisha ripoti kuhusu hali ya sasa ya mwenendo unaostawi wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwamba: Kuimarishwa ushirikiano na kuwepo mawasiliano ni njia bora itakayosaidia kukabiliana na vikwazo na maamuzi ya kiuchumi ya upande mmoja ya Marekani dhidi ya nchi huru duniani. 

Katika mazungumzo hayo, Sergei Lavrov aidha amebainisha kwa kina kuhusu ushirikiano wa Tehran na Moscow katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na sekta ya uchumi na kusisitiza kuwa nchi yake iko tayari na ina hamu ya kupandisha juu kiwango cha ushirkiano kati yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kufikia kiwango cha kimkakati. Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameashiria umuhimu wa uanachama wa Iran katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Shanghai na  na kusema: Russia inaunga mkono kupanda nafasi ya Iran katika jumuiya hiyo. 

 

Tags