Jun 25, 2022 04:21 UTC
  • Raeisi: Iran ni mshirika endelevu wa BRICS katika nishati

Rais Ebrahim Raeisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran inaweza kuwa mshirika endelevu wa kuunganisha nchi wanachama wa BRICS katika maeneo muhimu ya kupitisha nishati na masoko makubwa duniani kwa kuzingatia nafasi yake ya kipekee ya jiografia ya kisiasa na jiografia ya kiuchumi.

Rais Ebrahim Raeisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran inaweza kuwa mshirika endelevu wa kuunganisha nchi wanachama wa BRICS katika maeneo muhimu ya kupitisha nishati na masoko makubwa duniani kwa kuzingatia nafasi yake ya kipekee ya jiografia ya kisiasa na jiografia ya kiuchumi.

Akihutubu Ijumaa katika kikao kilichofanyika kwa njia ya intaneti cha Jukwaa la Kibiashara la BRICS, Raeisi amesema: “Tuko tayari kusaidia BRICS kufikia malengo yake kupitia uwezo wetu ikiwa ni pamoja na katika sekta za uchukuzi wenye bei nafuu, nguvu kazi yenye ujuzi pamoja na ustawi wetu wa kisayansi.”

Rais wa Iran amesema dunia ya sasa inakabiliwa na changamoto anuai na mpya ambazo zimeathiri urafiki na amani duniani. Raeisi amesisitiza haja ya kuimarisha maingiliano baina ya nchi za BRICS hasa kwa kuzingatia migogoro mipya duniani kama vile janga la corona, mabadiliko ya tabia nchi na mizozo ya kimataifa.

Rais Raeisi akihutubia kikao cha BRICS kwa njia ya intaneti

Rais Raeisi amesema sera kinzani katika masuala ya kimataifa, sera za kujichukulia maamuzi ya kimataifa bila kuwashirikisha wengine, utaifa, na changamoto kama vile vikwazo ni nukta zinazoashiria ulazima wa kuunda taasisi mpya zenye nguvu pembizoni mwa Umoja wa Mataifa ili kuwezesha kupatikana jamii ya mwanadamu yenye mustakabali wa pamoja na wakati huo huo kulinda mamlka ya kujitawala nchi.

Raeisi amesema BRICS ni kundi ambalo limechukua hatua ya kwanza kufikia lengo hilo kwani linajumuisha nchi zinazoibuka kiuchumi na ambazo zina ubunifu mpya katika masuala ya kimataifa.

Amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaamini kuhusu ulazima wa kuwa na uadilifu duniani sambamba na kusisitiza kuwa kuna ulazima wa nukta hiyo kujadiliwa katika ngazi ya kimataifa.

Kundi la BRICS linajumuisha Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini. Nchi hizo kwa pamoja zina asilimia 40 ya watu wote duniani na zina robo ya pato ghafi lote duniani.

 

Tags