Jun 26, 2022 14:40 UTC
  • Rais wa Iran afanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Iraq mjini Tehran

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mchana wa leo amemlaki rasmi Waziri Mkuu wa Iraq hapa Tehran.

Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo Jumapili amemlaki rasmi Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al Kadhimi katika ikulu ya Saad- Abad hapa Tehran. Waziri Mkuu wa Iraq leo adhuhuri amewasili Tehran akiongoza ujumbe wa kidiplomasia wa nchi yake na kupokewa na Ali Akbar Mehrabian Waziri wa Nishati wa Iran. 

Baada ya kulakiwa katika ikulu ya Saad- Abad,  Rais Ebrahim Raisi wa Iran baadaye alikuwa na mkutano na Waziri Mkuu wa Iraq na waandishi wa habari.  Rais wa Iran amesema katika mkutano huo wa pamoja na waaandishi wa habari kuwa: hatua mpya zimepangwa kuchukuliwa ili kuwezesha uhusiano wa kifedha kati ya Tehran na Baghdad. 

Image Caption

Rais Sayyid Ebrahim Raisi na Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al Kadhimi jana Jumapili walishiriki katika mkutano huo na waandishi wa habari baada ya mazungumzo ya pande mbili. Rais Raisi amesema katika mkutano huo kuwa, anamkaribisha  al Kadhimi na ujumbe wake wa ngazi ya juu katika ziara yao hapa nchini. Uhusiano wetu na Iraq si uhusiano wa kawaida na kijadi  bali ni uhusiano mkubwa na mkongwe, na kuna azma ya kustawisha zaidi uhusiano kati ya nchi mbili. 

Rais Ebrahim Raisi ameongeza kuwa, "katika kupanua siasa za mahusiano na nchi jirani,  leo hii tunaiona Iraq kuwa taifa la karibu zaidi na taifa la Iran; aidha tuna uhusiano mkubwa na Iraq miongoni mwa nchi jirani .  

Tags