Jun 27, 2022 08:06 UTC
  • Wazayuni wameingiwa na hofu kutokana na safari ya Mkuu wa Sera za Nje wa EU Tehran

Waziri wa mambo ya nje wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, ambaye kila mara amekuwa akifanya uafriti na kuweka pingamizi dhidi ya mpango wa kuiondolea Iran vikwazo vya kidhalimu, ametoa matamshi ya uropokaji ya kukosoa safari ya Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya hapa mjini Tehran.

Siku ya Jumatatu, Josep Borrell, mkuu wa sera za nje wa EU aliwasili mjini Tehran katika kuendeleza juhudi za kuanzisha tena mazungumzo kuhusiana na faili la nyuklia la Iran ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na maafisa kadhaa wa Jamhuri ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa televisheni ya Al-Mayadeen, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kuwa yametokea majibizano makali ya maneno kati ya waziri wa mambo ya nje wa utawala wa Kizayuni Yair Lapid na mkuu wa sera za nje za Umoja wa Ulaya Josep Borrell kwa sababu ya safari aliyofanya Borrell mjini Tehran kwa lengo la kuanzisha tena mazungumzo ya nyuklia na Iran.

Lapid amekosoa vikali safari ya mkuu wa sera za nje wa EU mjini Tehran katika hali ambayo, tangu ilipoingia madarakani serikali ya waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni Naftali Bennett, afisa huyo wa Kizayuni hajaacha kutumia kila fursa aliyopata kukwamisha mchakato wa mazungumzo yanayolenga kuondoa vikwazo ilivyowekewa Iran.../

 

Tags