Jul 03, 2022 07:59 UTC
  • Jenerali Baqeri: Iran inafuatilia nyendo zote za maadui mipakani

Kamanda Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza usalama imara na thabiti katika mipaka ya magharibi ya nchi hii na kusisitiza kuwa, Iran inafuatilia kwa jicho la karibu nyendo na harakati za kutilia shaka za maadui muda wote.

Meja Jenerali Mohammad Hossein Baqeri ameyasema hayo leo Jumapili alipoutembelea mkoa wa magharibi wa Kurdistan na kuongeza kuwa, "Vyombo vyetu vya kiintelijensia, usalama na jeshi vipo macho na vinafuatilia kwa karibu sana harakati za kificho na siri za maadui."

Jenerali Baqeri amesema vikosi vya ulinzi na usalama katika mipaka ya Iran vinafuatilia muda wote harakati za maadui kupitia angani na nchi kavu, na kwamba hatua yoyote ya makosa ya adui itakabiliwa na jibu kali la taifa hili.

Vikosi vya Wanamaji vya Iran

Mkuu huyo wa Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, "Harakati na nyendo ghalati za adui katika eneo hazifichiki machoni petu."

Meja Jenerali Mohammad Hossein Baqeri mwezi Aprili mwaka huu alisisitiza kuwa, tishio lolote la adui, na kwa kiwango chochote, litapata jibu kali la kuumiza la Jamhuri ya Kiislamu, mpaka limfanye adui ajute.

Tags