Jul 03, 2022 09:14 UTC
  • Ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kuhusu jinai za Marekani

Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa ujumbe wa Twitter kwa mnasaba wa kukumbuka jinai ya meli ya kivita ya Marekani iliyotungua ndege ya abiria ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Ghuba ya Uajemi.

Ujumbe huo umeambataisha taarifa za jinai hiyo ya kuogofya na kuwaenzi waliouawa shahidi katika tukio hilo.

Katika takwimu ya Iran tarehe 27 Juni hadi tatu Julai hutambuliwa kama Wiki ya Haki za Binadamu za Kimarekani ambapo katika wiki hii utambulisho halisi wa jinai za Marekani hubainishwa wazi mbele ya walimwengu na hivyo kufichua hadaa ya Marekani katika madai yake kuwa eti ni mtetezi wa haki za binadamu. Katika wiki hii pia huangaziwa zaidi jinai za Marekani dhidi ya Wairani wasio na hatia.

Moja ya jinai za Marekani dhidi ya watu wa Iran ilijiri miaka 34 iliyopita ambapo ndege ya abiria aina ya Airbus ya shirika la ndege la Iran iliyokuwa ikitoka Bandar Abbas, kusini mwa Iran kuelekea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu, ilishambuliwa kwa makombora mawili ya jeshi la Marekani kwenye maji ya Ghuba ya Uajemi. Manowari ya kijeshi ya Marekani USS Vincennes ilifyatua makombora hayo na kuua shahidi watu wote 298 waliokuwa katika ndege hiyo. Shambulio hilo lilidhihirisha zaidi unyama wa serikali ya Marekani. Viongozi wa Marekani walizidisha ukatili wao pale walipomzawadia medali ya ushujaa nahodha wa meli hiyo kutokana na kitendo hicho kilichochukuliwa na serikali ya Washington kuwa cha ushujaa.

Mmoja wa wanafamilia wa waliouawa wakati meli ya kivita ya Marekan ilipotungua ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la Iran Air akiwa katika eneo la tukio wakati wa kumbukumbu ya jinai hiyo

Historia ya miongo ya karibuni inaonyesha kuwa, Marekani na waitifaki wake ni wakiukaji wakubwa zaidi wa haki za binadamu duniani kwa kuanzisha vita katika maeneo mbali mbali duniani hasa eneo la Asia Magharibi. Vita hivyo vya Marekani vimesababisha matatizo makubwa na kupelekea idadi kubwa ya raia, hasa wanawake na watoto kupoteza maisha huku wengi wakiendelea kukumbwa na masaibu. 'Wiki ya Haki za Binadamu za Marekani' ni wakati muafaka wa kufichua jinai hzo za Marekani duniani.

Tags