Jul 03, 2022 09:24 UTC
  • Iran yakamilisha oparesheni ya kuwatuma waumini kwenda Hija

Mkuu wa oparesheni ya kuwabeba Wairani wanaoenda kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu amesema oparesheni hiyo inakamilika usiku wa leo.

Gholareza Rostamian mkuu wa oparesheni ya Hija katika viwanja vya ndege vya Iran ametoa taarifa kuhusu mchakato mzima wa kuwabeba Mahujaji kuelekea Saudia na kusema: "Tokea tuanzishe oparesheni ya kuwabebe waumini kuekelea Hija, hadi sasa safari za ndege 16o zimeshaondoka nchini Iran kuelekea Madina na Jeddah na leo safari hizo zitafika 162."

Mwaka huu, wakuu wa Saudia wameidhinisha Wairani 39,635 kutekeleza ibada ya Hija. 

Rostamian ametangaza kuwa safari zote hizo za ndege za kuwatuma Mahujaji wa Iran nchini Saudia zimetekelezwa na Shirika la Ndege la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Aidha amesema oparesheni ya kuwarejesha Mahujaji Wairani itaanza tarehe 14 Juni.

Mamia ya maelefu ya waumini wa dini tukufu ya Kiislamu kutoka kona zote za dunia wameendelea kuwasili nchini Saudia, wakiwa ni miongoni mwa Waislamu milioni moja wanaotarajiwa kushiriki ibada ya Hija mwaka huu wa 2022 ambapo hii ni mara ya kwanza baada ya miaka miwili ya kuzuiwa mahujaji kutoka nje ya Saudia kutekeleza ibada hiyo mhimu kutokana na janga la Covid.

Waumini wakiwa katika Msikiti Mtakatifu wa Makka

Ni raia elfu chache tu wa Saudia na wakaazi wa kigeni nchini humo ndio waliruhusiwa kuhudhuria Hija ya kila mwaka katika miaka miwili iliyopita wakati Covid-19 ilisababisha matatizo katika usafiri duniani.

Mwaka huu ni Waislamu milioni moja tu watakaotekeleza ibada ya Hija, chini ya nusu ya viwango vya kabla ya Covid, na wanaoruhusiwa ni wenye umri wa miaka 18 hadi 65 ambao wamechanjwa kikamilifu na hawana magonjwa sugu. Waumini wataendelea kuingia Saudia kabla ya kuanza rasmi ibada ya Hija siku chache zijazo.

Tags