Jul 17, 2022 11:51 UTC
  • Marandi: Makubaliano ya Marekani na Iran ni hatua erevu ya kuzuia mgogoro wa nishati

Mohammad Marandi, mchambuzi mwandamizi wa masuala ya kisiasa na mitaala kuhusu Marekani amesema makubaliano kati ya Marekani na Iran ni hatua erevu ambayo kama itachukuliwa itazuia kutokea mgogoro wa nishati katika nchi za Magharibi.

Marandi ameongeza kuwa Iran inapenda kufikia mwafaka na Marekani, lakini inapasa Wamarekani watoe fursa kadhaa pia za upendeleo kwa sababu haiwezekani wao watake kila kitu.

Kwa mujibu wa mtaalamu huyo wa masuala ya kisiasa, vyombo vya habari vya Magharibi vimedai kuwa, mkwamo uliojitokeza katika kufikia mwafaka na Iran umesababishwa na takwa la Tehran la kuondolewa jina la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kwenye orodha ya Marekani ya "mashirika ya kigaidi", ilhali Iran haijashurutisha katu suala hilo.

Marandi amebainisha kuwa, Marekani haiko katika nafasi ya kuweza kuchukua hatua dhidi ya Iran na ndio maana chaguo bora kwake ni kufikia makubaliano na kuruhusu mafuta ghafi ya Iran yaingie kwenye soko la Ulaya.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Sputnik, tangu Novemba 2021, na katika mazungumzo na Marekani na waitifaki wake wa Magharibi, Iran imekuwa ikisisitizia kuondolewa vikwazo vyote vya kidhalimu ilivyowekewa ambavyo vinakwamisha kutekelezwa kikamilifu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ambalo ni sharti la utanguilizi kwa mwafaka wowote ule .../ 

Tags