Jul 31, 2022 11:43 UTC
  • Mapigano yazuka baina ya askari wa mpakani wa Iran na wapiganaji wa Taliban

Gavana wa mji wa Hirmand ulioko kaskazini ya mkoa wa Sistan na Baluchistan kusini mashariki mwa Iran amesema, yamezuka mapigano kati ya askari wa kikosi cha mpakani cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wapiganaji wa kundi la Taliban la Afghanistan.

Meysam Barazandeh, Gavana wa mji wa Hirmand ulioko mkoani Sistan na Baluchistan ameliambia shirika la habari la IRNA kuwa, leo mchana yamezuka mapigano baina ya askari wa ulinzi wa mpakani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na vikosi vya kundi la Taliban katika eneo la Shaghalak kwenye mji wa Hirmand.

Kwa mujibu wa Barazandeh, taarifa zaidi zitatolewa baadaye kuhusu sababu ya kuzuka mapigano hayo na kama kuna maafa yoyote yaliyotokea.

Askari wa mpakani wa Iran

Kwa mara kadhaa sasa zinazuka tofauti na mapigano kama hayo kati ya pande mbili, kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni kutokuwa na uelewa na kwa sababu ya uzoefu mdogo walionao askari wa mpakani wa Taiban juu ya masuala ya mipaka kati ya Iran na Afghanistan.

Kundi la Taliban lilitwaa tena madaraka ya nchi Afghanistan mwezi Agosti 2021 baada ya askari wa jeshi vamizi la Marekani na waitifaki wake kuondoka kwa mpigo nchini humo na rais Ashraf Ghani kuikimbia nchi.../

Tags