Aug 06, 2022 11:33 UTC
  • Kustawisha mabadilishano ya kibiashara na nchi za Kiafrika ni katika vipaumbele vya Iran

Hamid Forozan Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Kimataifa wa Wizara ya Ushirikiano, Kazi na Ustawi wa Jamii ya Iran amesisitiza kuwa, uwezo wa nchi za Kiafrika umeandaa msingi mzuri wa kustawisha biashara na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kikao cha Uratibu cha Mkutano wa Kwanza wa Kamisheni ya Pamoja ya Iran na Burundi kimefanyika kwa kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Masuala ya Kimataifa katika Wizara ya Ushirikiano, Kazi na Ustawi wa Jamii ya Iran na wawakilishi wa taasisi na mashirika yaliyo chini ya wizara hiyo.  

Kikao cha Kamisheni ya Pamoja ya Iran na Burundi huko nyuma kiliwahi kufanyika chini ya usimamizi wa Wizara ya Ushirikiano, Kazi na Ustawi wa Jamii ya Iran na kusainiwa hati saba za ushirikiano katika masuala mbalimbali kama ya kuondoa viza kwa pasi za kusafiria za kidiplomasia, huduma za kilimo, kuunga mkono uwekezaji baina ya serikali mbili, kushirikiana kibiashara, afya na matibabu pamoja na mafunzo ya kiufundi na kitaalamu.   

Hamid Forozan Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Kimataifa wa Wizara ya Ushirikiano, Kazi na Ustawi wa Jamii ya Iran amesema leo katika kikao cha Kamisheni ya Pamoja ya Iran na Burundi kwamba: mapato makubwa ya Burundi yanayotokana na sekta ya kilimo na sambamba na sekta hiyo, moja ya kadhia muhimu sana ni uchimbaji wa almasi nchini humo ambao unaweza kuwa fursa nzuri kwa ajili ya kushirikiana Burundi na Iran katika uwanja huo.  

Tags