Aug 08, 2022 03:44 UTC
  • Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Qatar wazungumzia jinai za Israel dhidi ya Wapalestina

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amefanya mazungumzo na mwenzake wa Qatar na kusema: "Harakati za Mapambano (muqawama) zina mpango kamili wa kutoa jibu kali na lenye taathira kwa jinai za utawala wa Kizayuni."

Hossein Amir-Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran jana Jumpili alifanya mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al Thani  ambapo wamejadili matukio ya hivi karibuni ya Ukanda wa Gaza na hali jumla ya eneo la Asia Magharibi.

Tokea Ijumaa maeneo kadhaa ya Ukanda wa Ghaza yamekuwa yakikabiliwa na mashambulizi ya kuogofya na ya kinyma ya utawala wa Kizayuni wa Israel. Kufuatia jinai hiyo ya Wazayuni, Brigedi ya Quds, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Jihad Islami imevurumisha maroketi katika maeneo kadhaa ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kuusababishia hasara kubwa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iran, IRNA, katika mazungumzo na mwenzake wa Qatar, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amelaani vikali uvamizi wa kikatili wa utawala ghasibu wa Kizayuni ambao umewaua shahidi makumi ya wanawake na watoto wa Kipalestina. Amesema Israel ni mwanzilishi wa mashambulizi ya hivi karibuni ya kijeshi na hilo linatokana na utambulisho wake wa kichokozi na kivamizi.

Watoto ni waathirika wakuu wa jinai za Israel huko Gaza

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameitaja hatua ya utawala wa Kizayuni ya kutaka  Msikiti wa Al-Aqsa uhujumiwe kuwa ni ya uchochezi.

Katika mazungumzo hayo ya simu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar aidha amelaani uchokozi wa hivi karibuni  wa utawala dhalimu wa Israel huku akiashiria juhudi za kusimamisha vita amesema hatua ya kichochezi ya utawala ghasibu wa Israel katika Msikiti wa Al-Aqsa ni sababu ya kushadidi mgogogoro na makabiliano ya hivi karibuni ya kijeshi.

Tags