Aug 11, 2022 07:54 UTC
  • Jeshi la Majini la Iran lazima shambulio la maharamia Bahari Nyekundu

Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetangaza kuwa makomandoo wa jeshi hilo wamezima hujuma ya maharamia dhidi ya meli ya kibiashara ya Iran katika Bahari Nyekundu.

Admeli Mostafa Tajeddini, Naibu Kamanda wa Operesheni za Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema meli hiyo ya mizigo ya Iran ilishambuliwa na maharamia wasiojulikana na baada ya kuomba msaada wa dharura, manowari ya kivita ya Iran iliyokuwa karibu ilifika haraka eneo la tukio na kupambana na kuwatimua maharamia.

Amesema: Shukrani kwa uwepo athirifu (wa vikosi vyetu vya baharini), baada ya makabiliano makali, boti zilizokuwa zikishambulia zimetoroka.

Naibu Kamanda wa operesheni za Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema operesheni hiyo imeongozwa na manowari ya Jamaran iliyoundwa na wataalamu wa hapa nchini.

Meli hiyo ya mizigo ya kibiashara ya Iran sasa inaelekea ilikokuwa ikienda baada ya kunusuriwa na makomando hao ambao wako katika Msafara wa Manoari za Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Boti ya kijeshi ya mwendokasi ya Iran

Tokea mwaka 2008, Jeshi la Iran limekuwa likilinda doria katika Ghuba ya Aden ili kulinda meli za mizigo na meli za mafuta za Iran na za nchi zingine. Hatua hiyo ya Iran kutuma meli zake katika eneo hilo ni kwa mujibu wa jitihada za kimataifa za kukabiliana na maharamia.

Tokea wakati huo Iran imefanikiwa kuzima hujuma kadhaa za maharamia dhidi ya meli zake na zile za kigeni.

Tags