Aug 16, 2022 13:58 UTC
  • Iran kuimarisha zaidi uhusiano na Mauritius

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hussein Amir-Abdollahian amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inakaribisha ustawishaji uhusiano na Mauritius.

Ameyasema hayo leo mjini Tehran katika mkutano na Waziri wa Leba wa Mauritius Soodesh Satkam Callichurn.

Katika mkutano huo, Amir-Abdollahian amesema nchi  mbili zinaweza kuimarisha uhusiano zaidi katika sekta za biashara, uchumi, kilimo, na utalii.

Aidha amesema Iran iko tayari kuunda tume ya pamoja ya kiuchumi baina ya nchi mbili.

Kwa upande wake Callichurn amesema Mauritius inataka kustawisha ushirikiano na Iran katika nyanja zote.

Mkutano wa Waziri wa Mafuta wa Iran na Waziri wa Leba wa Mauritius 

Jana pia waziri huyo wa leba wa Mauritius alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mafuta wa Iran Javad Owji ambapo walijadili ushirikiano wa nchi mbili katika sekta ya nishati.

Kikao cha kwanza cha ushirikiano wa kiuchumi baina ya Iran na Mauritius kilifanyika Jumapili mjini Tehran kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kibiashara baina ya nchi mbili ambapo mapatano ya ushirikiano pia yalitiwa saini.