Aug 20, 2022 03:51 UTC
  • Iran yatoa pongezi kufuatia kufanyika uchaguzi wenye mafanikio Kenya

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza wananchi na serikali ya Kenya kwa kufanyika kwa mafanakio uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.

Jumanne Agosti 9 kulifanyika uchaguzi mkuu nchini Kenya ambapo katika uchaguzi wa rais William Ruto alitangazwa mshindi kwa kupata asilimia 50.49 ya kura zilizopigwa huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Raila Odinga aliyepata asilimia 48.85 ya kura zote zilizopigwa. Hata hivyo Odinga amepinga matokeo hayo na amesema atawasilisha malalamiko mahakamani akitaka matokeo yabatilishwe. Rais wa sasa Uhuru Kenyatta hakugombea kwani anamaliza muhula wake wa pili kisheria baada ya kuingia madarakani mwaka 2013.

William Ruto ametangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi Kenya (IEBC) kuwa mshindi katika uchaguzi wa rais

Kwa msingi huo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Nasser Kan'ani Chafi ametuma salamu za pongezi kufuatia kufanyika uchaguzi nchini Kenya huku akipongeza nafasi ya serikali, vyama, wanasiasa, viongozi wa kikabila na kidini nchini humo katika kufanikisha uchaguzi huo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema uchaguzi huo wa Kenya ni mfano na uzoefu uliofanikiwa katika eneo na bara zima la Afrika.

Kan'ani Chafi ameelezea matumaini yake kuwa mchakato wa kisiasa wa kuundwa serikali ya nchi hiyo utafuata mkondo wa matakwa na malengo ya wananchi.

Tags