Sep 16, 2022 13:08 UTC
  • Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Muqawama wa Palestina na Yemen ni muendelezo wa mapambano ya Ashura

Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesisitiza kuwa, muqawama wa Palestina na Yemen ni muendeleza wa mapambano ya Ashura katika jangwa la Karbala mwaka 61 Hijria.

Hujjatul Islam Sayyid Mohammad‑Hassan Aboutorabi Fard amesema hayo kwenye khutba za ibada hiyo ya kisiasa na kimaanawi iliyosaliwa katika Chuo Kikuu cha Tehran na huku akizungumzia kufikia kileleni Arubaini ya Imam Husain AS huko Iraq kesho Jumamosi na falsafa ya mapambano ya Imam Husain AS ya kupambana na dhulma, ubeberu na udikteta amesema, kutotetereka wapiganaji jihadi wa Yemen na Palestina na nchi nyingine katika mapambano yao dhidi ya dhulma, ubeberu na uistikbari leo hii, ni muendelezo wa mapambano hayo ya Imam Husain AS dhidi ya watawala madhalimu na madikteta.

Vile vile amezungumzia jinsi wananchi wa Iraq wanavyoonesha ukarimu mkubwa kwa wafanyaziara ya Arubaini ya Imam Husain AS sasa hivi na kuongeza kuwa, ukarimu tunaoushuhudia Iraq hivi sasa kwa kweli ni jambo la kujivunia.

Mashaya, matembezi ya Arubaini ya Imam Husain AS yanayoendelea nchini Iraq hivi sasa

 

Khatibu huyo wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran pia amesema, Arubaini ya Imam Husain AS ni nembo ya kudhihirisha mapenzi makubwa; wapenzi wa uadilifu na ubinadamu duniani kwa mpendwa wa wapigania uhuru na ukombozi kote ulimwenguni yaani Imam Husain AS. 

Ameongeza kuwa, inabidi uzoefu uliopoatikana katika kusimamia na kuendesha kwa ufanisi wa hali ya juu Arubaini ya mwaka huu ya Imam Husain AS utumiwe vizuri kwa ajili ya kimarisha umoja na mshikamano katika umma mzima wa Kiislamu na hususan kati ya mataifa mawili ya Iran na Iraq.

Tags