Sep 22, 2022 02:07 UTC
  • Meja Jenerali Safavi: Vita vya kulazimishwa vya Iraq dhidi ya Iran viliweza kutabirika lakini havikuweza kuzuiwa

Msaidizi na Mshauri mwandamizi wa Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema vita vya kulazimishwa vilivyoanzishwa na Iraq dhidi ya Iran viliweza kutabirika lakini haikuwezekana kuzuiwa.

Leo Alhamisi Septemba 22 inasadifiana na siku ya kukumbuka kuanza vita vya kulazimishwa vilivyoanzishwa na utawala wa Baath wa Iraq dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Jeshi vamizi la utawala wa Saddam(dikteta wa zamani wa Iraq) tarehe 31 mwezi Shahrivar mwaka 1359 sawa na mwezi Septemba mwaka 1980 huku likidhani kwamba lingefanikiwa kuiteka Tehran ndani ya  wiki moja liliishambulia vikali Iran kwa kustafidi na kila aina ya silaha. Tarehe 31 mwezi Shahrivar inatambulika katika kalenda ya minasaba ya Iran kuwa ni siku ya kuanza Wiki ya Kujihami Kutakatifu; ambapo katika wiki hiyo moja marasimu mbalimbali hufanyika katika Iran nzima ya Kiislamu. 

Shirika la habari la Iran, IRNA limeripoti kuwa, Meja Jenerali Sayyid Yahya Rahim Safavi Msaidizi na Mshauri mwandamizi wa Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana Jumatano alisema katika hafla ya kumbukumbu ya Wiki ya Kujihami Kutakatifu mjini Tehran kwamba: " Dikteta Saddam Hussein aliyepinduliwa huko Iraq alikuwa na fikra za kuivamia Iran kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu; na katika njia hiyo alikuwa na uhakika wa kuungwa mkono na kupewa baraka zote na serikali za Marekani, Umoja wa Kisovieti na baadhi ya nchi za Kiarabu katika eneo. 

Dikteta Saddam Hussein 

Msaidizi na Mshauri mwandamizi wa Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Saddam hata hivyo hakutimiza hata lengo lake moja na ukweli ni kuwa, Saddam na pande zote zilizounga mkono vita hivyo vya kulazimisha dhidi ya taifa la Iran ziligonga mwamba. Amesema baadaye serikali ya dikteta Saddam Hussein ilipinduliwa na utawala dhalimu sana kama wa Wamarekani;  katika hali ambayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sasa inatambulika kama  dola  lenye nguvu katika eneo. 

Tags