Sep 23, 2022 07:56 UTC
  • Rais Raisi aondoka New York na kurejea Tehran

Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo Ijumaa ameondoka jijini New York, Marekani na kuelekea Tehran baada ya kushiriki katika Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Rais Sayyid Ebrahim Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo ameondoka New York na kurejea Tehran baada ya kushiriki na kuhutubia katika Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kuhudhuria pia katika vikao kuhusu mabadiliko ya kielimu katika shirika la UNESCO, na kukutana na kuzungumza na baadhi ya viongozi wa dini, wataalamu na wachambuzi wa siasa za Nje za Marekani, baada ya kukukutana maafisa wa ngazi ya juu wa vyombo vya habari vya Marekani, kuhojiwa na vyombo mbalimbali vya habari na kuzungumza na Wairani wanaoishi Marekani.  

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aidha kwa mara ya kwanza ameshiriki katika mkutano wa 77 wa viongozi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York.  Kuonekana kwa mara ya kwanza Rais wa Iran katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kulikwenda sambamba na ubunifu maalumu na kupandisha taswira ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani; suala ambalo lilibadilika haraka na kuwa habari muhimu ili kwa mara nyingine tena dunia iweze kushuhudia jinai hiyo ya Marekani na nia ya Iran katika kufuatilia jinai hiyo. 

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika ujumbe wake mkuu aliotoa kuhusu uadilifu na kupinga dhulma na ukandamizaji; na kutolea mfano masuala ya haki za binadamu, ugaidi na  kadhia ya nyuklia. Amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwa katika njia ya kulinda uhuru wake itafanikisha malengo yake yote licha ya gharama zote katika miongo minne iliyopita na itaendeleza njia yake hiyo. 

Rais Ebrahim Rais alipata fursa pia ya kukutana na kuzungumza kwa nyakati tofauti na viongozi mbalimbali wa nchi na shakhsia wa kimataifa huko New York akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres. 

Rais Ebrahim Rais na Antonio Guterres mjini New York 

 

Tags