Sep 24, 2022 14:15 UTC
  • Rais Raisi asisitiza ulazima wa kuwachukulia hatua kali wavurugaji usalama na utulivu wa nchi

Rais Ebrahim Raisi amezungumza na familia ya Shahidi Mohammad Rasool Dust Mohammadi na kusisitiza ulazima wa kuwachukulia hatua kali wavurugaji usalama na utulivu wa nchi.

Shahidi Muhammad Rasool Dust Mohammadi amekuwa mmoja wa Mashahidi wa usalama na wapiganaji walinzi wa haram katika mji mtukufu wa Mashhad, baada ya kufikia daraja ya juu na tukufu ya kufa shahidi katika machafuko yaliyotokea siku ya Jumatano katika mji huo.
 
Wakati wananchi wengi wa Iran wameguswa na kusikitishwa na kifo cha Mahsa Amini na hivi sasa wanasubiri kutangazwa matokeo ya uchunguzi wa sababu ya kifo chake, imefanyika mikusanyiko ya malalamiko na upinzani katika baadhi ya miji ukiwemo wa Tehran ambayo imesababisha uharibifu wa mali za umma.
 
Katika ghasia hizo, magari ya utoaji huduma, ya kubebea wagonjwa na ya Zimamoto nayo pia hayajasalimika na mashambulio ya wazusha machafuko na wavurugaji amani, kiasi kwamba hadi sasa mafundi kadhaa wa kada ya tiba na watoaji huduma za misaada wamejeruhiwa na kulazwa hospitalini, na magari 61 ya kubebea wagonjwa yameharibiwa.
Shahidi Muhammad Rasool Dust Mohammadi

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametilia mkazo kuchukuliwa hatua kali wavurugaji usalama na utulivu wa nchi, na akaeleza kwamba: kujitokeza kighera Shahidi Dust Mohammadi kwenye medani ya kulinda usalama kumedhihirisha jinsi Shahidi huyo alivyokuwa muelewa wa zama, mwaminifu kwa uongozi wa kidini na mzalendo wa kweli.

 
Leo mara baada ya kuwasili nchini akitokea New York Umoja wa Mataifa, Sayyid Ebrahim Raisi alifanya mazungumzo ya simu na familia ya Shahidi Dust Mohammadi, ambapo mbali na kuifariji na kuipa mkono wa pole familia ya shahidi huyo mtukufu, alisisitiza pia kufuatiliwa na kuchukuliwa hatua kali waliosababisha kifo chake.
 
Rais Raisi amesisitiza ulazima wa kutofautishwa kati ya maandamano ya malalamiko na uvurugaji nidhamu na usalama wa jamii na akasema, kujitokeza matukio kama yaliyopelekea kuuawa shahidi Dust Mohammadi ni ufanyaji fujo na uovu, na akaviagiza vyombo husika kuwachukulia hatua kali wavurugaji usalama, utulivu wa nchi na wa wananchi.../