Sep 27, 2022 04:43 UTC
  • Bagheri Kani: Wanaowekea dawa vikwazo kivipi wana wasiwasi kuhusu haki za binadamu nchini Iran

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Anayehusika na Masuala ya Kisiasa amesisitiza wale wote wanaoziwekea dawa vikwazo iweje wana wasiwasi kuhusu haki za binadamu hapa nchini.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya siku zote wamekuwa kimya huku wakiunga mkono sera za ikulu ya Marekani (White House) kuhusu taathira za vikwazo vya maisha ya raia wa Iran.  Viongozi hao wa Ulaya aidha wamedhihirisha na kuwaunga mkono wazusha fujo na machafuko yaliyoshuhudiwa siku kadhaa zilizopita hapa nchini na kudai kuwa, vikwazo dhidi ya Iran vitekelezwe." 

Ali Bagheri Khani Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Anayehusika na Masuala ya Kisiasa amesisitiza kuhusu vigezo vya undumakuwili vinavyotumiwa na Umoja wa Ulaya kuhusu haki za binadamu na kuandika katika ukurasa wake wa twitter kwamba: nchi za Ulaya ambazo zinakataa kuiuzia Iran dawa mbalimbali za matibabu nahivyo kusababisha vifo vya watoto wasio na hatia hapa nchini kwa namna ipi zinaweza kutiwa wasiwasi na suala la haki za binadamu nchini Iran? 

Shirika la habari la Iran, IRNA limeripoti kuwa Bagheri Kani jana Jumatatu alituma ujumbe katika mtandao wake wa twitter kwamba: kukaa kimya na kutowajibika ipasavyo Umoja wa Ulaya mkabala wa vikwazo vya upande mmoja na haramu vya Marekani na wakati huo huo kukiukwa pakubwa haki za binadamu za wananchi wasio na hatia wa Iran; kulikoashiriwa katika ripoti ya ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kunaonyesha mienendo na vigezo vya undumakuwili vya taasisi hiyo ya Ulaya kuhusu masuala ya haki za binadamu. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Anayehusika na Masuala ya Kisiasa aidha ameongeza kuwa: nchi za Ulaya ambazo zinakataa hata kuiuzia Iran dawa na vifaa mahsusi vya kupunguza makali na maumivu kwa watoto wanaougua ugonjwa wa ngozi wa kipepeo na hivyo kusababisha kuaga dunia watoto hao wasio na hatia haziwezi kutiwa wasiwasi na hali ya haki za binadamu nchini Iran.

Ugonjwa wa kipepeo na kukosa dawa watoto hapa nchini