Sep 28, 2022 02:18 UTC
  • Kubadilishwa ghafla faili la kesi ya Mahsa Amini kuwa mradi wa mapinduzi dhidi ya serikali

Kwa kuzingatia kuwa utawala haramu wa Israel uliamuru hadharani kuuawa kigaidi Shirin Abu Akleh, mwandishi wa habari wa Kipalestina wa televisheni ya al-Jazeera, Mkristo ambaye pia alikuwa na uraia wa Marekani akiwa kazini huko Jenin, na ambapo umeshindwa kuhalalisha kitendo hicho, hivyo umeamua kukaa kimya kwa sasa kuhusu kifo cha Mahsa Amini.

Pamoja na hayo ni wazi kuwa utawala huo wa kigaidi ndio unaonufaika zaidi na maandamano ya kichochezi yaliyoibuliwa nchini Iran kufuatia kifo cha binti wa Kiirani Mahsa Amini na kuna uwezekano mkubwa kwamba vyombo vingi vya habari vya lugha ya Kifarsi, ambavyo kwa sasa vinachochea ghasia na vurugu nchini hapa vinafanya hivyo kwa udhamini wa kifedha wa utawala huo.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na mjadala muhimu kati ya maadui sugu wa Iran na baadhi ya washirika wao wa kieneo, kuhusu jinsi ya kukabiliana na nguvu inayozidi kuongezeka kieneo ya Iran, na iwapo wanapaswa kuanza kukabiliana na Iran ndani ya ardhi yake yenyewe au kupitia washirika wake wa kieneo katika mrengo wa mapambano. Kumekuwepo na mitazamo miwili kuhusiana na suala hilo. Wa kwanza ni 'Muhimili wa Joka' ambao ulitolewa na Saud al-Faisal, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, na wa pili ni nadharia ya "Pweza" ambayo iliyotolewa na Naftali Bennett, Waziri Mkuu wa zamani wa utawala wa Kizayuni, ambaye hadi miezi michache iliyopita alikuwa akilishikilia madaraka ya utawala huo katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Uharibifu uliofanywa na magenge ya uhalifu kwa kisingizio cha kulalamikia kifo cha Mahsa Amini

Nadharia zote mbili ni sawa kabisa kimuundo ila tu zinatofautiana kimatamshi. Mjadala daima umekuwa ni kwamba je, zimwi hilo bandia kwanza linapaswa kukatwa kichwa au mikono na miguu? Mjadala huo katika siku za nyuma ulipelekea kutolewa kipaumbele kwa mbinu za kijeshi dhidi ya Iran na washirika wake katika eneo, mbinu ambazo hata hivyo sio tu zilishindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa bali hata zilikuwa na matokeo kinyume na ilivyopangwa kama tunavyoshuhudia hilo katika sehemu nyingi, mifano ya karibuni zaidi ikiwa nchini Syria na Yemen. Kwa hivyo, katika hatua zilizofuata, muundo jumla wa nadharia zote mbili uliachwa kama ulivyo, lakini njia za utekelezaji wake zilibadilishwa kutoka zana ngumu za kijeshi hadi programu laini, na kulingana na mazingira, juhudi zilifanywa kwa ajili ya kuanzisha migogoro na changamoto tofauti nchini Iran au katika nchi rafiki.

Katika uwanja huo, njama nyingi zilianzishwa nchini Iraq na Lebanon ambazo zilipelekea kuondolewa madarakani kwa serikali halali ya Adel Abdul Mahdi huko Iraq na nafasi yake kuchukuliwa na serikali iliyoteuliwa ya Mustafa Kadhimi, ambayo hadi leo bado iko madarakani licha ya kupita karibu mwaka mmoja tangu uchaguzi ufanyike, na hali ya mambo huko Lebanon pia inafanana na hiyo hiyo ya Iraq. Kwa hakika matukio yaliyotokea nchini hapa siku chache zilizopita kwa kisingizio cha kufuatilia kifo cha Mahsa Amini yanawiana na malengo na maslahi ya maadui wa Jamhuri ya Kiislamu. La sivyo, kama kweli lengo lilikuwa ni kutetea haki za wanawake au kujua ukweli kuhusu kifo cha Mahsa Amini basi hatua ambazo zingechukuliwa na waibuaghasia nchini ni kufuata mkondo wa sheria ambao ungesaidia kufikiwa lengo hilo haraka na sio kuzua ghasia, machafuko na mauaji nchini.

Kwa vyo vyote vile, Tel Aviv na waitifaki wake wa Magharibi na Saudia ndio washindi na wanufaika wakuu wa kupotoshwa ghafla mkondo wa malalamiko kuhusu kifo cha Mahsa Amini na kugeuzwa kuwa machafuko na uharibifu nchini Iran, jambo ambalo bila shaka halikutokea hivi hivi tu bali lilikuwa limepangwa vizuri tangu mwanzo. Kifo hicho cha kusikitisha kilitokea mara tu baada ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kupewa uanachama rasmi katika mkutano wa 22 wa Jumuiya Shanghai huko Samarkand nchini Uzbekistan.

Wakati huo huo, mkutano wa 77 wa viongozi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ulikuwa unaendelea huko New York baada ya kumalizika virusi vya corona, ambapo uwepo huko wa viongozi na maafisa wa ngazi za juu wa pande zinazohusika na suala zima la nyuklia la Iran, uliutia wasiwasi mkubwa utawala wa Kizayuni, kwa sababu kabla ya utawala huo kuingilia mazungumzo ya Vienna, kulitangazwa kuwa makubaliano kati ya pande hizo yalikuwa yanakaribia kufikiwa na hata kulikuwepo na uwezekano wa kufikiwa makubaliano ya mwisho pambizoni mwa mkutano wa Baraza Kuu.

Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu alifika nyumbani kwa wazazi wa Mahsa Amini kuomboleza kifo chake

Kuna masuala mengine matatu ambayo yamezidisha wasiwasi wa utawala huo. La kwanza, ni kuimarika uwepo wa Iran nchini Syria baada ya kupunguzwa uwepo wa Russia kufuatia vita vya Ukraine; pili ni kuanza intifadha mpya huko Palestina, ambayo kimsingi inatokana na utawala wa kibaguzi wa Israel kukiuka utekelezaji wa maazimio na mapatano ya amani ya Umoja wa Mataifa na tatu ni kuingia Hizbollah ya Lebanon katika uwanja wa gesi ya Karish katika Bahari ya Mediterania jambo ambalo limeuzuia utawala huo kupora na kuhodhi nishati hiyo katika eneo hilo linalozozaniwa.

Kwa kuzingatia mambo hayo, tunaweza kusemwa kwamba kifo cha Mahsa Amini na mkondo wa sheria ambao unapasa kufuatwa ni suala moja, na mradi wa kupindua serikali ambao unafuatwa na maadui wa Iran kuhusu kadhia hiyo ni suala tofauti kabisa, ambapo kutenganishwa masuala mawili hayo kunaweza kusaidia pakubwa katika kufahamika vyema matukio yanayojiri sasa nchini Iran na katika eneo zima la Asia Magharibi.