Sep 28, 2022 08:17 UTC
  • Jen. Safavi: Sera ya muqawama inazidi kuimarika na kupata nguvu

Mshauri Mkuu wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, stratejia ya muqawama katika eneo hili la Asia Magharibi na miongoni mwa mataifa yanayopenda haki duniani inazidi kuimarika na kupata nguvu, na bila shaka nguvu hizo zitafelisha njama za kambi ya ubeberu.

Meja Jenerali Yahya Rahim Safavi alisema hayo jana Jumanne pambizoni mwa Maonyesho ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Damghan na kuongeza kuwa, maana nyingine ya muqawama ni kuungana mataifa kuunda taifa moja.

Amebainisha kuwa, "Stratejia ya muqawama ni kubadilisha mlingano wa nguvu katika mfumo wa kimataifa, na Mapinduzi ya Kiislamu yaliweka msingi wa kuundwa na kupanuliwa muqawama kote duniani, kwa kutoa muhanga mashahidi laki tano na maveterani."

Meja Jenerali Safavi ameeleza bayana kuwa, ushindi mtawalia wa Wapalestina dhidi ya utawala wa Kizayuni ni matunda ya chuo cha muqawama.

I

Mshauri huyo Mkuu wa Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran aidha amesema, matukio mbalimbali, michakato na mikakati tofauti ya Iran katika kipindi cha takriban miaka 40 iliyopita, ni kuelekea kwenye kuongeza kadiri inavyowezeka nguvu zake za kitaifa. 

Meja Jenerali Safavi ameongeza kuwa, Sera ya muqawama inazidi kuimarika na kupata nguvu, na hakuna shaka itasambaratisha ubabe wa mataifa ya kibeberu yanayotaka kudhibiti mashirika yote ya kimataifa.

Tags