Sep 29, 2022 12:06 UTC
  • IRGC yashambulia kwa makombora ya balestiki ngome za magaidi kaskazini mwa Iraq

Vikosi vya Nchi Kavu vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) vimeanzisha duru mpya ya mashambulio dhidi ya ngome na maficho ya magaidi kwa kutumia makombora ya balestiki huko kaskazini mwa Iraq.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, jeshi la SEPAH limetumia makombora 360 yenye kupiga shabaha kwa usahahi mkubwa katika operesheni hizo dhidi ya ngome na maficho ya magaidi kwa kutumia makombora ya balestiki na droni katika eneo la Kurdistan, kaskazini mwa Iraq.

Amesema ngome 42 za magaidi hao, baadhi zikiwa zimepishana kwa umbali wa kilomita 400 zimesambaratishwa na kuharibiwa kikamilifu na makombora hayo ya balestiki na droni za Iran.

Brigedia Jenerali Mohammad Pakpour, Kamanda wa Vikosi vya Nchi Kavu vya Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema vikosi hivyo vilitumia makombora 73 ya balestiki na makumi ya droni za kamikaze katika operesheni ya jana Jumatano.

IRGC imesema katika taarifa kuwa, magaidi hao wa Kikurdi kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakivuka mpaka na kuingia nchini Iran, na kushambulia vituo vya mipakani.

Brigedia Jenerali Mohammad Pakpour

Jeshi la SEPAH limesema litaendeleza operesheni hizo zilizoanza tokea Jumamosi iliyopita, kwa shabaha ya kulinda mipaka ya nchi hii na usalama wa wananchi wa Iran.

Magaidi hao wametumia maandamano ya fujo hapa Iran kuendeleza harakati zao katika miji ya Wakurdi ndani ya ardhi ya Iran, na kuwasha moto wa ghasia, mbali na kufanya mashambulio ya umwagaji damu.

Tags