Oct 02, 2022 02:18 UTC
  • Mwakilishi wa Iran mjini Geneva: Mauaji ya kizazi katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu imekuwa sera ya kudumu ya utawala wa Israel

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva amesisitiza kuwa, mauaji ya kizazi katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu imekuwa sera ya kudumu na ya makusudi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Ali Bahraini, balozi mpya na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva amesema katika kikao cha Baraza la Haki za Binadamu kuhusiana na ukiukwaji wa haki za binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu kwamba Wapalestina bado wanakabiliana na ukiukwaji mkubwa zaidi wa muda mrefu wa haki za binadamu na wako chini ya udhibiti wa mfumo wa kibaguzi wa apartheid ya kijeshi.

Bahraini ameongeza kuwa: Utumiaji nguvu za kijeshi kwa ajili ya kuwaua Wapalestina, unyanyasaji, mauaji ya kizazi, upanuzi wa vitongoji haramu vya walowezi na adhabu za umati vimekuwa mbinu ya kudumu na sera ya ukandamizaji wa makusudi ya utawala wa Kizayuni tangu mwanzo mwa kuvamiwa na kukaliwa kwa mabavu Palestina.

Bahraini amesema, baadi ya nchi zimekuwa na mienendo ya kinafiki na zinajigamba kuwa vinara wa kutetea haki za binadamu ilhali zinaendelea kunyamazia kimya uhalifu unaofanyika Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Askari wa Israel akimkaba koo mtoto wa Kipalestina

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva ameongeza kuwa: Nchi hizo kwa hakika ni "washirika" katika kutenda jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na zinapaswa kuwajibishwa sambamba wahusika wa ubaguzi wa rangi (apartheid) unaofanywa na utawala huo huko Palestina  

Tags