Oct 02, 2022 07:42 UTC
  • Salami: Suala la kisasi cha mashahidi wa 'Ijumaa Nyeusi' lipo kwenye ajenda

Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesisitiza kuwa, vikosi vya jeshi hilo vitalipiza kisasi cha kuuawa shahidi makumi ya watu wakiwemo maafisa usalama katika Ijumaa Nyeusi huko mjini Zahedan, katika mkoa wa Sistan na Baluchestan kusini mwa Iran.

Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda wa IRGC sambamba na kutoa mkono wa pole kufuatia shambulio la kigaidi lililopelekea makumi ya watu kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa mjini Zahedan Ijumaa iliyopita amebainisha kuwa, vita dhidi ya mamluki wa kigeni waliojipenyeza humu nchini vitaendelea kwa nguvu zote.

Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amewapongeza na kuwashukuru wakazi wa mji wa Zahedan kwa kushirikiana kuzima njama hizo za maadui wa taifa hili.

Kamanda Salami ameeleza bayana kuwa: Tunawahakikishia wakazi wenye subira wa mkoa huu (Sistan na Baluchestan) kwamba mapambano endelevu dhidi ya njama za mabeberu wa ulimwengu na magaidi mamluki waliokodishwa na vyombo vya usalama vya maajinabi yataendelea.

Taarifa ya jana ya IRGC ilisema kuwa, SEPAH itashirikiana na vikosi vingine vya usalama, sera na intelijensia kutoa jibu kali kwa mamluki waliohusika na ghasia hizo za umwagaji damu, wakilenga kupanda mbegu za chuki na kufanya jinai.

Mji wa Zahedan mkoani Sistan na Baluchestan

Kwa mujibu wa Gavana wa Mkoa wa Sistan na Baluchestan kusini mwa Iran, Hussein Modarres Khiabani, watu 21 waliuawa shahidi huku wengine zaidi ya 20 wakijeruhiwa katika vitendo hivyo vya kigaidi vya Ijumaa ya juzi katika mji wa Zahedan, makao makuu ya mkoa huo wa kusini mwa nchi.

Alisema, wapiganaji kadhaa wenye mafungamano na makundi ya kigaidi na yanayotaka kujitenga, walivamia kituo cha polisi na kurusha mawe na kufyatua risasi, jambo lililokabiliwa na jibu la polisi.

 

Tags